Join Our Groups
TOPIC 4: KUTUNGA KAZI ZA
FASIHI ANDISHI
UTUNGAJI WA MASHAIRI
Utungaji/uandishi
wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma mtunzi ili atunge kazi
yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo vinamsumbua akilini na
kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka aliwasilishe wazo lake ili hadhira
ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi hukosa usingizi na hivyo hulazimika
kuamka na kuandika kile kinachomsukuma akilini mwake.
Mambo ya Kuzingatia
katika Utungaji wa Mashairi
Uandishi
wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna
milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi,
na kuonja.
1. Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani
mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje –
je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
2. Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu
gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako
ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?
3. Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi
nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini
mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?
4. Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni
unaonjaje – ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au
sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?
5. Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje?
Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya?
Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?
Uzoefu wa Mwandishi
Uzoefu
ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi
ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo
gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana
nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) kuna baadhi
ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana nailoni na je
kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?
Uchunguzi/utafiti
Uchunguzi
unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa.
Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi
zake. Uchunguzi ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje,
anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje
na wenzane na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi
kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na
akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.
Mwandshi
baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi yake. Hapa sisi
tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika hatua ya
utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya hapo
tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo yatatuwezesha
kutunga mashairi.
DHANA YA SHAIRI
Shairi
ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari.
Sauti za silabi hufanana
zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta
ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.
Mpango
wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na
burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi
ijapokuwa hazikuandikwa
Mashairi
yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika
mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo kadhaa yanayotakiwa
kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:
1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho
kina uzani sawa.
2. Vina – Ni mwisho wa mistari ambayo huwa
na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa sentensi.
3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi
katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.
4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti.
Kuna vituo vya aina tatu:Kituo cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo
hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni
kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo
nusu bahari – ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu
hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.
Katika
mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na
maana kamili.
Vipengele vya Fani
katika Mashairi
- Jina
/ anwani
- Mandhari
- Wahusika
- Muundo
–tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k
- Mtindo
– pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha
mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.
Vipengele vya Maudhui
katika Mashairi
- Vipengele
vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo, mtazamo, na
dhamira za mwandishi.
- Matumizi
ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza, kufundisha,
kuburudisha, kukosoa, na kadharika.
Baada
ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.
EmoticonEmoticon