Join Our Groups
TOPIC 6: UFAHAMU
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Ufahamu
wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo
wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna
fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza
humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena
kwa maneno yake mwenyewe.
Kujibu Maswali ya
Habari Uliyosikiliza
Ufahamu
wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya
kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
- Kuelewa
vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
- Kuelewa
vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
- Kuelewa
sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
1.
Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila
anachokisema.
2.
Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo
jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
3.
Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili
kumasidia kukumbuka hapo baadae.
4.
Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha
kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia
kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
Kufupisha Habari
Ili
kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyoisikiliza yafuatayo hayana budi
kuzingatiwa; kusikiliza habari kwa makini ili kuielewa vizuri, kuandika mawazo
makuu yanayojitokeza katika kila aya, kuyaunganisha mawazo makuu na kuiandika
habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno kama inazidi na kuandika idadi
hiyo mwisho wa ufupisho upande wa kulia chini kidogo.
Zoezi
Soma
habari kisha toa ufupisho wake
UFAHAMU WA KUSOMA
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu
anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti.
Kujibu Maswali
kutokana na Habari ndefu uliyosoma
Kuna
vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
- Uelewa
wa msamiati na
- Uelewa
wa matini
Ili
kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati
uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka
vilevile matini yote hataeleweka.
Katika ufahamu wa
kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au
kitabu inatakiwa ajiulize, Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa
analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi
itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama
za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na
endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
3. Kubaini maana ya maneno na misemo
mbalimbali;
habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini
maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa
vyema maana ya mwandishi.
4.
Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele
anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa
kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma
na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
Kufupisha Habari
Kufupisha
habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache lakini bila
kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.
Ufupisho
wa habari huwa na sifa hizi:
- Huwa
ni mfupi kuliko habari ya mwanzo
- Huwa
na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya mwanzo
- Hujumuisha
mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka kwenye habari ya mwanzo
- Mawazo
haya sharti yapangwe katika mtririko wenye mantiki
Ufahamu wa Kusoma |
Hatua za Kufuata
katika Kuandika Ufupisho
Ili
kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti zifuatwe:
1.
Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili kuielewa vizuri
2.
Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya
3.
Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa
maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana ya habari ya kwanza.
4.
Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi
iliyotakiwa.
5.
Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili
kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
Kufupisha Habari ndefu
uliyosoma
Ili
kuweza kuandika ufupisho wa habari ndefu uliyoisoma hatua zifuatazo sharti
zifuatwe, kusoma habari kwa makini na kuielewa vizuri, kubaini mawazo makuu,
kuandika ufupisho wa habari kwa maneno yako, kuhesabu idadi ya maneno na
kupunguza yaliyozidi na kupitia tena habari ya mwanzo na ya mwisho kama muda
unaruhusu. Aidha ufupisho wa habari huwa ni mfupi na una ujumbe uleule wa
habari ya mwanzo.
EmoticonEmoticon