Join Our Groups
TOPIC 5: USIMULIZI
Usimulizi ni jumla ya maelezo
yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Katika mada hii
utajifunza juu ya taratibu za usimulizi wa matukio kupitia njia kuu mbili za
masimulizi, yaani kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi. Pia utaweza
kujifunza juu ya mbinu mbalimbali za usimulizi.
USIMULIZI WA HADITHI
Usimulizi
hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia ya
masimulizi ya mdomo. Kila njia hutegemea namna msimuliaji anavyoweza
kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana,
njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa mfano kama utahitaji kumweleza
mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi,
yaani utatumia njia ya kumwandikia barua. Lakini kama unamsimulia mtu ambaye
yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.
|
USIMULIZI WA HABARI
Taratibu
za Usimulizi wa Matukio:
Usimulizi
wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao
hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo
muhimu ambayo yatawawezesha watu hao kulielewa tukio linalosimuliwa sawasawa na
huyo anayeshuhudia.
Mambo muhimu ya kutaja
katika usimulizi wa matukio ni pamoja na haya yafuatayo:
1. Aina ya tukio – msimuliaji atatakiwa kubainisha
katika maelezo yake aina ya tukio. Kwa mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya
barabarani au mkutano.
2. Mahali pa tukio
– ili
msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni lazima kumwelewesha ni
mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjini inafaa kutaja hata
jina la mtaa.
3. Wakati – katika usimulizi ni muhimu pia
kutaja muda ambao tukio limetendeka kama ni asubuhi, mchana au jioni bila
kusahau kutaja muda halisi yaani ilikuwa saa ngapi.
3. Wahusika wa tukio
– ni
muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani, wingi wao, jinsia yao, umri wao n.k.
4. Chanzo cha tukio
–
kila tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika usimulizi.
5. Athari za tukio
–
athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali, je watu wangapi
wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.
6. Hatima ya tukio
–
msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe baada ya tukio kutokea na
kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa mfano, kama tukio ni ajali ya
barabarani hatima yake inaweza kuwa majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva
aliyehusika kukamatwa.
Usimuliaji wa Habari |
Kwa
hiyo misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na sehemu kuu
tatu:
a) Utangulizi – sehemu hii huwa na maelezo tu ya
utangulizi ambayo hulenga kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji au
wasikilizaji. Kwa kawaida utangulizi wa tukio huwa ni maneno machache kiasi
yasiyozidi aya moja.
b) Kiini – kiini cha usimulizi huelezea tukio
halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, muda, mahali na athari za tukio.
c) Mwisho
– mwisho
wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio linalohusika,
wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maelezo ya msimuliaji
kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.
Usimuliaji wa Habari |
Mbinu za Usimulizi
Ili
habari inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za
kusimulia katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake.
Baadhi
ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi
ya Kiswahili.
1.
Kwa upande wa uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na
tukio ambalo anasimulia. Nayo ni kama vile milio, sauti na matendo.
2.
Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti
usimulizi huo uwe na kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa
kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.
Kwa
vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa
katika wakati uliopita.
EmoticonEmoticon