Join Our Groups
TOPIC 7: UANDISHI WA
BARUA
Uandishi Wa Barua
Barua
za kirafiki ambazo pia huitwa za kidugu huandikwa baina ya watu wa undugu au
jamii moja. Katika mada hii utaweza kujifunza muundo wa uandishi wa barua ya
kirafiki na jinsi ya kuandika barua ya kirafiki. Utaweza kutofautisha kati ya
barua ya kirafiki na ile isiyokuwa ya kirafiki.
BARUA ZA KIRAFIKI
Iwapo
ni katika ndugu barua za kirafiki zaweza kuwa kwa watu kama: baba, mama,
shangazi, mume, mke, mtoto, na kadhalika. Katika jamii waandikiwao barua za
kirafiki ni kama jirani, rafiki, mpenzi, mwalimu, mwanafunzi, daktari, mgonjwa,
na kadhalika.
Muundo wa Barua za
Kirafiki
Mambo
muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa barua za kirafiki:
1.
ANWANI kamili ya mwandishi, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa
karatasi.
2.
TAREHE, chini ya anwani.
3.
MTAJO wa heshima kwa anayeandikiwa, kama vile, mpendwa, mpenzi, na kadhalika,
huandikwa kushoto, baada ya tarehe.
4.
UTANGULIZI wa barua yenyewe ambao kwa desturi huwa ni salamu.
5.
BARUA YENYEWE ambayo ndiyo kiini cha waraka.
6.
SALAMU za kumalizia, pengine kwa jamaa na jamii.
7.
HITIMISHO, katika aya, maalumu ambayo huwa, kwa mfano: ‘Ni mimi baba yako
akupendaye, na kadhalika.
8.
SAHIHI ambayo si sharti wala muhimu sana.
9.
JINA au MAJINA ya mwandishi, mwishoni.
Kuandika Barua |
Tazama mfano wa barua ya kirafiki:
Mfano 1
MUSOMA
FISH PACK
S.L.P
4546
MUSOMA
23/5/2013
Mwanangu
Nyamchele,
Ninafuraha
kukujulisha kuwa nimepokea barua yako. Mambo yote uliyoyaeleza nimeyaelewa
barabara. Huku nyumbani sote tu wazima na ni matumaini yetu kwamba afya yako ni
nzuri.
Tabia
ya kulalamikia chakula ni mbaya. Tabia kama hii ikikomaa husababisha ulafi.
Kumbuka hukwenda shuleni kula kama nguruwe. Huko shuleni nimekupeleka ili usome
kwa bidii na ujifunze mengi. Usitamani kustarehe na kufikiria maakuli na anasa
zingine za ulimwengu huu. Ondoa fikira za chakula akilini mwako na uache
uzembe, eboo!
Hebu
nikuonye kuhusu kuwapima na kuwachagua walimu. Walimu katika shule hiyo ni
wabobezi na ndio maana nikakupeleka hapo. Wanajua mnayostahili kufundishwa.
Huna ruhusa ya kusema eti walimu wengine ni wakali na hufundisha haraka haraka
sana. Wewe unahitaji kutega sikio na kutii. Ukiwa makini na uwe na imani
utayaelewa mambo unayofundishwa. Usisahau kuwa mchagua jembe si mkulima.
Mambo
makubwa unayostahili kuyatilia bidii ni masomo yako. Muda wa miaka minne ni
mfupi sana. Uonyeshe adabu njema kila wakati. Uwaonyeshe walimu wako taadhima
na uwatii daima dawamu.
Jambo
lililo kubwa katika shughuli yoyote ni uvumilivu. Ukivumilia utavuna matunda mabivu.
Sitachoka kukusisitizia, ‘Ukilima pantosha, utavuna pankwisha.’ Fanya kila
jitihada utimize mambo mengi iwezekanavyo kuanzia leo lakini usipapie chochote.
Ndo ndo ndo hujaza ndoo.
Mungu
akubariki. Umwombe akusaidie katika kila jambo. Ujiepushe na maovu yoyote yale.
Ukiwa na jambo usiwe na hofu kutuarifu mara moja. Mama yako amekusalimu sana.
Amenikumbusha nikupashe hakuna refu lisilo na ncha.
Kwaheri
kwa sasa.
Ni
mimi, baba yako akupendaye,
Magafu
Malima
Thanks for the good work you are doing to support online studies
ReplyDeleteGood job
ReplyDelete