Join Our Groups
TOPIC
2: MJENGO WA TUNGO
Maana ya Tungo
Tungo
ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio
vidogovidogo vilivyo chini yake. Au tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho
hudokeza taarifa fulani ambayo huweza kuwa kamili au isiyo kamili.
Kwa
maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda
neno, neno kuunda kirai, kirai kunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama
tulivyokwisha kuona hapo juu tungo huanzia neno; rejea aina za tungo.
AINA ZA TUNGO
Tungo neno: Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi
ya neno ambayo ni mofimu au fonimu.
Mfano; anacheza, kakimbia.
Tungo Kirai: ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini
ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
Mfano;
mtoto mzuri, kiyama chake, bondeni
Tungo kishazi:
Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha
ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea
chenyewe.
KIRAI NA UAINISHAJI
WAKE
Dhana
ya kirai itaeleweka vizuri kwa kuzingatia sifa zake zifuatazo:
1.
Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika; yaani ni kipashio
kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo
zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.
2.
Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika.
3.
Kirai ni tungo, yaani ni aina moja wapo ya tungo, aina nyingine za tungo ni
neno, kishazi na sentensi.
4.
Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili.
5.
Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika katika
sarufi ya lugha husika. Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika
kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Kirai huweza kutokea upande wowote,
wa kiima au kiarifu katika sentensi. Kirai ni kikubwa kuliko neno
Kama
tulivyobainisha hapo juu aina ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo
chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.
1. Kirai nomino (KN);
Ni
kirai ambapo neno lake kuu ni nomino. Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa
kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.
2. Kirai kitenzi (KT); Kirai-kitenzi ni kirai ambacho
kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya Kitenzi na neno au mafungu
mengine ya maneno. Hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya virai huwa ni
kitenzi.
3. Kirai kivumishi
(KV); Kirai-kivumishi ni kirai ambacho
muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa kawaida muundo huu huwa ni wa
kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho.
4. Kirai Kielezi (KE); Tofauti na aina nyingine ya virai
miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya
neno kuu (yaani kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala
yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika
Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua
zaidi neno hilo.
5. Virai viunganishi
(KV);
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kwa na katika,
au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine kirai
hicho ni kile ambacho neno kuu ni kiunganishi.
TUNGO KISHAZI
Kishazi
ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe
uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea
chenyewe.
Sifa za Kishazi
1.
Kishazi hupatikana katika/ ndani ya sentensi.
2.
Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi,
haiwezi kuwa kishazi. Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi
tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi.
3.
Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika
muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa
kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi sahili” kikiwa
sentensi inayojitegemea.
4.
Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika muktadha
wa sentensi kuu.
5.
Vishazi vingi, hata vishazi huru huwa na kiima dhahiri.
6.
Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru huwa na kitenzi kimoja kikuu.
7.
Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika
kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.
8.
Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi.
9.
Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi
lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana.Kishazi huwa na kiarifu kimoja
na kiima kimoja, Lakini sentensi huweza kuwa na kiima kimoja.
AINA ZA VISHAZI
1. Vishazi huru: Kishazi huru ni kishazi
kinachotaewaliwa ka kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili
usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata
kikiondolewa katika muktadha wa sentensi ambamo vimejikita huweza kujitegemea
kama sentensi.
2. Vishazi tegemezi:
Kishazi
huru ni kishazi kinachotawaliwa ka kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake
hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa.
Kishazi tegemezi peke yake hakitoi ujumbe unaojitosheleza
Sifa za Kishazi Tegemezi
1.
Kishazi tegegemezi hutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi huru.
2.
Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya
sentensi nzima.
3.
Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi vya utegemezi
4.
Vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi.
5.
Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa,
kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofu ya masharti n.k
Aina ya Vishazi Tegemezi
a)
Vishazi
tegemezi vivumishi
1. Vishazi
tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa.
2. Vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino
inayovumishwa
b)
Vishazi
tegemezi vielezi
1.
Vishazi tegemezi vya mahali
2.
Vishazi tegemezi vya wakati
3. Vishazi tegemezi vya namna au jinsi
4. Vishazi tegemezi vya masharti
5. Vishazi
tegemezi vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendo.
6.
Vishazi tegemezi vya sababu/chanzo
Dhima na Hadhi ya Vishazi
Kishazi
chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamili
inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali
hutegemea vishazi vingine. Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili).
Kishazi tegemezi hakina hadhi hii, vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi
vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi
huchukua dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni
dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.
UFAFANUZI WA AINA ZA TUNGO
Sentensi
Sentensi
ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na
kiarifu na kinacholeta maana kamili.
Sifa za Sentensi
Sentensi
lazima iwe na mpangilio wa maneno ambao unakubalika na wazungumzaji wa lugha
husika.
1.
Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo na kisarufi.
2.
Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu /huwa na kirai nomino na kirai
kitenzi.
3.
Sentensi huweza kuwa na zaidi ya kiima kimoja na kiarifu zaidi ya kimoja.
4.
Sentensi inaweza kuundwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
5.
Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi
kimoja au zaidi.
6.
Sentensi huonyesha hali mbalimbali, kama vile amri, ombi, mshangao, swali n.k
MUUNDO WA SENTENSI
Muundo
wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima unakuwa na vipengele vifuatavyo:
a) Kiima:
Ni
sehemu katika sentensi ambayo hujaza sehemu ya mtenda au mtendwa wa jambo
linaloelezwa. Katika tungo kiima hutokea kushoto mwa kitenzi.
b) Kiarifu:
Ni
sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayo arifu tendo lilofanywa,
linapofanywa au litakapofanywa. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika
sentensi ambayo wakati mwengine huweza kusimama pekee, kwani wakati mwingine
huchukua viwakilishi vya kiima.
Vipashio vya Kiima
- Nomino peke yake
-
Nomino, kiunganishi na nomino
- Nomino
na kivumishi
-
Kivumishi na nomino
- Kiwakilishi
peke yake
- Kiwakilishi
na kivumishi
- Nomino na kishazi tegemezi
vumishi
- Kitenzi
jina
- Nomino na vivumishi
zaidi ya kimoja
- Kitenzi jina na
nomino
- Umbo kapa
Taarifa zitolewazo na
kiarifu kuhusu kiima
- Kiima ni nani
-
Kiima kina nini
- Kiima hufanya nini
- Kiima
kinahisi nini
Sifa za kiarifu
- Huwa na kitenzi na pengine
huambatana na maneno mengine.
- Kiarifu
kwa kawaida huja baada ya kiima
Vipashio vya kiarifu
- Kitenzi kikuu peke yake.
-
Kitenzi kisaidizi au vitenzi visaidizi vilivyosambamba na kitenzi kikuu.
-
Kitenzi kishirikishi na kijalizo
- Yambwa
(shamirisho)
-
Kijazalio
-
Chagizo
Sifa za Chagizo
1.
Chagizo kwa kawaida huwa ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi
kama kielezi.
2.
Kwa kawaida ni vipashio vya ziada. Si lazima viwepo katika sentensi ili ijisimamie.
3.
Huwa cha lazima ikiwa kinafuata kitenzi kishiriki. Hali ikiwa hivyo, kinafnaya
kazi kama kijalizo.
4.
Hutumika kufafanua kitenzi/kivumishi /kielezi.
5.
Hutumika kujaliza kiima/kama kijalizo.
AINA ZA SENTENSI
Aina
za sentensi kimuundo ni pamoja na hzi zifuatazo:
1. SENTENSI
SAHILI
Ni
sentensi ambayo huundwa na kishazi huru kimoja. Sentensi ya aina hii huwa
inaelezea taarifa moja tu.
Mfano;
- Wanafuzi wanafanya
mtihani
-
Walinzi walitaka kunizuia nisiingie ndani.
Miundo ya sentensi
sahili
1.
Muundo wa kitenzi kikuu peke yake.
Mfano: Gari limeanguka
2.
Muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka (TS)
nisipate (T) utajiri
3.
Muundo wa vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’.
Mfano: John amekuwa
akiangalia TV kwa muda mrefu sana.
4.
Muundo wa kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa
Sifa za Sentensi Sahili
1.
Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa kuwa kinaeleweka.
2.
Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu na
kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo na chagizo.
3.
Haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana.
2. SENTENSI
CHANGAMANO
Hii
ni sentensi yenye kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au
zaidi. Sifa moja kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi
ambacho hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu wa
uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea kingine.
Sentensi
changamano ina muundo wenye vishazi virejeshi.
Mfano:
Gari
liliopinduka jana jioni halikuharibika hatata kidogo.
3. SENTENSI
AMBATANO
Hii
ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia
viunganishi kama vile likini, wala, au, na, nakadhalika.
Miundo ya sentensi
ambatano
1.
Miundo yenye sentensi sahili tu.
Mfano:
Mwalimu
anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
2.
Miundo yenye sentensi sahili na changamano.
Mfano:
Walinzi waliposhindwa polisi waliwasaidia
lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.
3.
Miundo yenye sentensi changamano tu.
Mfano:
Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu
hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.
4.
Miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.
UCHANGANUZI WA SENTENSI
Uchanganuzi
wa sentensi ni mchakoto unaohusika na kuchanganua vipashio vyote vinavyuonda
sentensi kuanzia ngazi ya kategoria ya neno. Katika kipengele hiki utaweza
kujifunza hatua muhimu za kuzingatia wakati wa uchanganuzi wa sentensi. Pia
utajifunza njia mbalimbali zinazotumika katika uchanganuzi wa sentensi.
Hatua za Uchanganuzi
wa Sentensi
1.
Kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sahili, changamano au ambatano.
2.
Kutaja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu au kirai nomino na kirai kitenzi.
3.
Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai
kitenzi.
4.
Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.
Njia za Uchanganuzi wa Sentensi
1.
Njia ya
Mishale/Mistari
Mfano
Uchanganuzi
wa sentensi kwa njia ya mishale
2.
Njia ya
Visanduku/Jedwali
Mfano:
3. Njia ya Matawi
Uchaganuzi
wa sentensi kwa njia ya matawi
Mifano
mingine ya uchanganuzi wa sentensi ambatano;
(Watu
wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti)
4. Njia ya Jedwali
Mfano:
Watu
wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti
5. Kwa Njia ya Matawi
Mfano:
Watu
wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti
6. Kwa Njia ya Mishale
Mfano:
Watu
wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti
asante kazi nzuri
ReplyDeleteAppreciate
ReplyDeleteKila kitu kimepangwa vizuri
ReplyDeleteVizuri sana
ReplyDeletevery good
ReplyDeleteIt is very nice
ReplyDelete