Join Our Groups
TOPIC 7: KUSOMA KWA UFAHAMU
KUSOMA KIMYA
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu
cha habari, kitabu au gazeti.
Maswali ya
Ufahamu kutokana na Habari uliyosoma
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatkiwa ajiluze, Je,
kinachoongelewa hapa nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi?
Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa
habari hiyo.
2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo
itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za
uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
3. Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji
kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia
kuelewa vyema maana ya mwandishi.
4. Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma,
kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari
aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma
KUFUPISHA HABARI
Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache
lakini bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.
Ufupisho wa habari
huwa na sifa hizi:
1. Huwa ni mfupi kuliko habari ya mwanzo
2. Huwa na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya
mwanzo
3. Hujumuisha mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka
kwenye habari ya mwanzo
4. Mawazo haya sharti yapangwe katika mtririko
wenye mantiki
Hatua za Kufuata katika Kuandika Ufupisho
Ili kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti
zifuatwe:
1. Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili
kuielewa vizuri
2. Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza
katika kila aya
3. Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au
kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana
ya habari ya kwanza.
4. Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili
kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi iliyotakiwa.
5. Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo
na pitia tena ufupisho ili kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
Kufupisha
Habari Uliyoisoma
Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii
ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa, mmoja akiwa amekatwa
kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa deni la Rupee kumi na tano
ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Polisi kaskazini mwa taifa hilo
wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana mfanyi biashara anayetokea jamii ya
hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao kwa kushindwa kulipa deni la biskuti
walizokuwa wamewachukulia watoto wao.
Mfanyi biashara huyo
amekamatwa.Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu
wa jamii ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa
kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo
'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika
lindi la umaskini .
Hata hivyo Visa vya ukatili wa
kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo
siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii
hiyo.
Zoezi
Kwa maneno yasiyozidi 30 fupisha habari uliyoisoma hapo juu.
EmoticonEmoticon