Join Our Groups
TOPIC 1:
UUNDAJI WA MANENO
Uundaji
wa maneno ni ujenzi au uzalishaji au utengenezaji wa maneno mapya. Uundaji wa
maneno mapya husaidia kuongeza msamiati katika lugha ili kukidhi mahitaji ya
mawasiliano. Uundaji wa maneno mapya husababishwa na mabadiliko ya kiuchumi,
kisiasa na kiutamaduni na maendeleo ya kisayansi yanayotokea katika jamii. Kwa
mfano tunayo maneno mapya, kama vile ufisadi, uwekezaji, ukeketaji,
ujasiriamali na mengine mengi kutokana na mabadiliko ya kijamii.
KUTUMIA UAMBISHAJI
Uambishaji
wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha
neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini
pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu
zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika
lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano 1
Wanapendana
= Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu
zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini
cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya
kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Angalia
mifano ifuatayo:
Neno
|
Viambisha
Awali
|
Kiini Viambisha
|
Tamati
|
Unapendelea
|
u-na-
|
-penda
|
el-e-a
|
Waliongozana
|
wa-li-
|
-ongoz-
|
an-a
|
Analima
|
a-na-
|
-lim-
|
-a
|
anayeiimbisha
|
a-na-ye
|
-imb-
|
-ish-a
|
Dhima za Mofimu
Baadhi
ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:
1.
Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana
katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini
au mzizi wake uleule. Mfano; Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza
kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile
fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.
2.
Uambishaji huonyesha nafsi
3.
Uambashaji huonyesha njeo (muda)
4.
Uambishaji huonyesha urejeshi
7.
Uambishaji huonyesha ukanushi
8.
Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi
Vitenzi
vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.
Vitenzi
|
Kiini
|
Nomino
|
Vitenzi
|
Cheza
|
-chez-
|
Mchezaji, mchezo
|
wanacheza/atamchezea
|
Piga
|
-pig-
|
Mpigaji, Mpiganaji
|
watanipiga, aliyempiga/wanaompiga
|
Uambishaji hutumika
kuzalisha viwakilishi na vielezi.
Neno (Kiwakilishi)
|
Kiini
|
Kielezi
|
Huyu,
Huyo
|
Hu
|
Humu, humo
|
Wangu,
wako,wake
|
wa
|
|
Hii,
hizo, hiki
|
hi
|
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.
Mfano:
Hawakulima
1.
Ha-, kiambishi cha ukanushi
2.
Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi
tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au
kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka
nk.
Dhima:Ukanusho,
kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.
Mfano
Neno
|
Viambishi Tamati
|
Anapiga
|
-a
|
Wanapigana
|
-an
|
Asipigwe
|
-w
|
Amempigisha
|
-ish-
|
Viambishi
tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na
vitenzi.
Neno
|
Kiini
|
Viambishi Tamati
|
Piga
|
pig-
|
-o
|
Mchezo
|
chez-
|
-o
|
Mtembezi
|
tembe-
|
-z-i
|
Mfiwa
|
-fi-
|
-us-a
|
KUTUMIA MNYUMBULIKO
Mnyumbulisho
ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu
wa kitu hicho.
Kunyumbua
katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili
kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia
kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.
Viambishi
vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa.
Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno
mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.
Pia
maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina,
kwa mfano:
Neno
|
Kiini
|
Shina
|
Maneno ya Mnyumbuliko
|
Elekea
|
elek
|
eleka
|
Elekeana, elekea, elekwa, elekesha
|
Shikishana
|
shik
|
shikisha
|
Shikishana, shikisha, shikishaneni
|
Kwa
ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi
au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi
mmoja wa maana.
Dhima ya Uambishaji na
Mnyambulikoa wa Maneno
Dhima
ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na
wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali
mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya
mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika
viambishi baada ya mzizi wa neno.
Kuunda Maneno
mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko
Uundaji
wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi
baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali
ya matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.
Zoezi 1
Unda
maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Tumia
maneno ya mnyambuliko katika
miktadha mablimbali
Maneno
ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo
hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda,
kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka,
kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.
Zoezi 2
Tumia
maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbal
EmoticonEmoticon