Join Our Groups
TOPIC 5: UTUNGAJI WA KAZI ZA KIFASIHI
Kazi
za fasihi simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga
kazi fulani ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni
mbalimbli zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa
ya kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile
ngonjera, methali, nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza pia kanuni
zinazoongoza utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.
MASHAIRI
Kanuni za Utungaji wa
Mashairi
Uandishi
wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna
milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi,
na kuonja.
1. Kuona: je, mhusika unayemfikiria kichwani
mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje –
je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
2. Kunusa: pua zako zinakufanya usikie harufu
gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako
ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?
3. Kuhisi: je, unapokaa karibu naye unajihisi
nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini
mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?
4. Kuonja: je, ukiweka kitu hicho mdomoni
unaonjaje – ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au
sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?
5. Kusikia: je, sauti unayoisikia ikoje?
Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni
nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki
je, iko chini au juu (kelele)?
Uzoefu wa Mwandishi
Uzoefu
ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi
ana uzoefu (uzoevu) wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo
gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana
nayo katika maisha yako? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) kuna baadhi
ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania? Magodoro haya yana nailoni na je
kama yasingekuwa na nailoni? Uzoevu/uzoefu wako ukoje?
Uchunguzi/utafiti
Uchunguzi
unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa.
Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi
zake.
Uchunguzi
ili ufahamu au ujue mtu, mnyama, mdudu na kadhalika – anatembeaje, anakulaje,
analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na wenzane
na mazingira yake? Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi kufanya
utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na
akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.
Mwandishi
baada ya kuzingatia mambo haya sasa anaweza kuanza kutunga kazi yake. Hapa sisi
tutajikita zaidi katika utunzi wa mashairi. Kabala hatujaenda katika hatua ya
utunzi ni muhimu kujua dhana ya shairi kwa ujumla wake, na baada ya hapo
tutakuwa tumekwisha pata maarifa yakutosha juu ya mashairi ambayo yatatuwezesha
kutunga mashairi.
Dhana ya Shairi
Shairi
ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari.
Sauti za silabi hufanana
zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta
ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.
Mpango
wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa hutoa picha wazi, maana halisi na
burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi
ijapokuwa hazikuandikwa.
Mashairi
yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika
mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi. Kuna mambo kadhaa yanayotakiwa
kufahamika kuhusu shairi, nayo ni:
1. Beti – Kifungu kimoja cha shairi ambacho
kina uzani sawa.
3. Mizani – Ni idadi zilizo sawa za silabi
katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.
4. Kituo – Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti.
Kuna vituo vya aina tatu:Kituo cha bahari – ni mstari unaotoka mwanzo
hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti;Kituo cha kimalizio – ni
kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti;Kituo
nusu bahari – ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu
hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.
Katika
mashairi (ya kimapokeo), kila mstari lazima uwe umekamilika na ubeti uwe na
maana kamili.
Vipengele vya Fani
katika Mashairi
Vipengele
vya fani katika shairi ni pamoja na:
1.
Jina / anwani
2.
Mandhari
3. Wahusika
4.
Muundo –tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k
Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.
Mtindo – pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.
Vipengele vya Maudhui
kati mashairi
1.
Vipengele vya maudhui ni pamoja na: migogoro, ujumbe, falsafa, msimamo,
mtazamo, na dhamira za mwandishi.
2.
Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza,
kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadharika.
Baada
ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.
Kuigiza Ngonjera
Katika
kuigiza ngonjera muigizaji hana budi kuzingatia fani yenye kanuni zifuatazo;
mtindo wa mashairi ya kimapokeo, muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani,
vina, vipande, mishororo na beti, kuteua mandhari kutegemeana na mada, kuwepo
kwa wahusika wawili au zaidi au makundi mawili au zaidi na matumizi ya lugha ya
kishairi.
Kanuni za Utungaji wa
Maigizo
Maigizo
ni tendo la kuiga sura, tabia, matendo na mazungumzo ya watu au viumbe wengine
yaani kuiga jinsi walivyoumbwa, wanavyotembea, wanavyovaa, wanavyosema n.k
Kanuni
na hatua za kutunga maigizo:
1. Kuchagua wazo,
tendo, visa au tukio la kuigizwa: Ni lazima jambo hilo liwe na uzito,
umuhimu au athari fulani katika jamii. Matukio hubainika kutokana na utafiti.
Matukio yanayoweza kuwa kiini cha kutungiwa maigizo ni kama vile matumizi
mabaya ya simu za mkononi, mitindo ya mavazi, madhara ya uganga wa kienyeji,
madhara ya UKIMWI n.k.
2. Kuchagua muktadha
au mahali pa kutendeka kwa jambo: Muktadha waweza kuwa ofisini, shuleni,
kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala n.k
3. Kuamua mtindo wa
kuwasilisha jambo la kuigizwa: Hapa mtunzi anaweza kutumia fumbo,
vichekesho, historia, tanzia n.k. Inashauriwa mtunzi kuchanganya mbinu ili
kuongeza mvuto.
4. Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo: Maudhui hujikita katika migogoro au
mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana pale migogoro inapofikia kilele. Kwa
mfano jamabazi sugu anapokamatwa.
5. Kuweka mpangilio
wa maonyesho: Maonyesho
hujumuisha vitendo na hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba aina moja au zaidi
ya maudhui. Sehemu kadhaa nazo hukaa zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo
mojawapo muhimu. Katika migawanyo hii yapasa mtunzi atunge kauli na vitendo
vinavyoandamana navyo.
6. Kubuni wahusika na
kuweka aina au idadi yao kulingana na matukio: Mtunzi anashauriwa kutumia wahusika
wanaohitilafiana. Kwa mfano wazee, vijana, wanawake, wanaume, wanene, wafupi
n.k. Mtunzi akishawateua anaweza kuwatungia kauli na zamu za matendo katika
sehemu mbalimbali.
7. Ni muhimu pia kwa
mtunzi kuwaumba wahusika wake na kuamua maleba yao: Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa
kuzingatia mazingira. Kwa mfano siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa
ngozi, kutumia mkongojo na kuvuta mtemba.
8. Urefu wa maigizo
ni suala la kuamliwa kutegemea tukio
9. Kutunga maelezo
kuhusu mandhari: Maumbile ya wahusika na vitendo vyao, ni muhimu kuelezwa
katika mabano.
10. Kuandika maigizo
na kuhariri: Ni
muhimu kutumia lugha ya kimazungumzo inayovutia, yenye kuleta taharuki na yenye
utamu unaoeleza maadili kwa mnato.
EmoticonEmoticon