Join Our Groups
TOPIC 6: UANDISHI
INSHA
ZA HOJA
Insha
za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo
zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo
analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea
msimamo wake.
Katika
uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo
analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zipate
kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi
kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana
msimamo gani kuhusu mada hiyo.
Muundo wa Insha za
Hoja
Katika
uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo:
1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile
ulichokijadili katika insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya
kulevya n.k
2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi
ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo
ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.
3. Kiini cha insha;
katika
kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako,
maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo
katika mjadala wako.
4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile
kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile
kilichohadiliwa katika insha.
BARUA RASMI
Dhima ya Barua Rasmi
Barua
rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa
taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa
kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.
Muundo wa Barua Rasmi
Barua
rasmi au barua ya kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa
kawaida huwa na sehemu zifuatazo:
1. Anwani ya
mwaandishi - huwekwa
juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa karatasi.
2. Tarehe ya barua
hiyo -
tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
3. Anuwani ya
mpokeaji -
Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa karatasi, na huwekwa
msitari mmoja chini ya tarehe.
4. Salamu - Chini ya anwani ya mpokeaji, barua
huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji
wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina
lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji
wa barua, tumia bw/bi
5. Mada - Kichwa cha barua rasmi huja pindi
tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti
kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa
kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.
6. Utangulizi – Hukaa chini kidogo ya mada ya
barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la
barua kama kidokezo.
7. Ujumbe - Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe
mfupi na unaotumia lugha rasmi.
8. Tamati – mwandishi humalizia kwa maneno ya
hitimisho kama vile: Wako mwaminifu, [jina], Sahihi
Kuandika barua rasmi |
SIMU
Dhima ya Simu ya
Maandishi
Simu
za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko
barua za kawaida. Simu hizo huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na
shirika la posta. Simu za maandishi hujulikana kama telegram. Kwa kawaida simu
za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi ni
njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako
ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu.
Gharama
za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa
hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama
kubwa.
Mfano
wa simu ya maandishi:
MUSA
KINGAMBE SLP 5299 DSM
NJOO
HARAKA
DADA
MGONJWA LINGIDO
Kuandika Simu za
Maandishi kwa Kuzingatia Muundo na Taratibu za Uandishi
Muundo
wa kuandika simu za maandishi una mambo yafuatayo ya kuzingatia ambayo ni
anwani ya mpelekewa taarifa, ujumbe na jina la mwandishi au mtuma simu. Mambo
mengine ya kuzingatia ni kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha
usomaji na kuandika simu ya maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa
na posta.
Simu |
Zoezi
Andika
simu za maandishi kwa kuzingatia muundo na taratibu za uandishi
Kadi
za mialiko ni aina ya karatasi ngumu zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba mtu
ahudhurie katika sherehe fulani kama vile harusi, ubatizo mahafali n.k
Muundo
wa Kadi ya Mialiko
Fafanua Muundo wa Kadi
ya Mialiko
Mambo
muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:
1.
Jina la mwandishi au mwalikaji
2.
Jina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi., Bw. Bw
&Bi n.k
3.
Lengo la mwaliko
4.
Mahali pa kufanyika shughuli
5.
Tarehe ya mwaliko
6.
Wakati wa shughuli
7.
Jina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibu.
Mialiko
huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa
katika kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile
Bwana….Bi…..au Ndugu…ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na
Bibi.
Kadi ya mwaliko |
Mfano wa Kadi ya
Mwaliko
Familia
ya Manyama na Joseph
Wanapenda
kukualika/kuwaalika Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye harusi
ya kijana wao mpendwa Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi
wa simba siku ya Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usiku
Kufika
kwako ndio mafanikio ya sherehe hii.
Majibu
kwa (wasiofika tu)
Emmanuel
Joseph
Simu:
0786 67 54 62
Kadi ya mwaliko |
UANDISHI WA DAYALOJIA
Dayalojia
ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa
kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utunagaji, dayalojia inaweza
kuwasilishwa kwa nijia ya mazungumzo au maandishi.
Katika
kutunga dayalojia mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia
hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia
dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na
kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano
kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na
mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.
Mambo ya kuzingatia
katika dayalojia ni pamoja na haya yafuatayo:
1.
Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha
2.
Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika
mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
3.
Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua
4.
Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia
iwe na uhalisia.
Dayalojia ya mazungumzo |
Mfano wa dayalojia
Wambura:
|
(Anaonekana
mwenye furaha,anamwita rafiki yake, Anna)Wow, Anna! Tumekutana
tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana wote wakiwa na nyuso za furaha).
|
Anna:
|
(Anatabasamu
huku ameshikilia mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu)Wambura! Bado unanikumbuka? Nina
furaha sana kwa kweli, ni muda mrefu sana.
|
Wambura:
|
(Anachekelea)Aaaah, nahisi kama naota Neema,
siamini kama nimekutana na wee leo hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa
kweli.
|
Anna:
|
(Anachekelea)
|
Wambura:
|
Mbona
wachekelea tu….
|
Dayalojia ya maandishi |
EmoticonEmoticon