Join Our Groups
TOPIC 8: UFAHAMU
Ufahamu
ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea
upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza
kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.
UFAHAMU WA KUSIKILIZA
Ufahamu
wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo
wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna
fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza
humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena
kwa maneno yake mwenyewe.
Kujibu Maswali ya
Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza
Ufahamu
wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile
kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:
1.
Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa
2.
Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza
3.
Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.
Katika ufahamu wa
kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo:
1.
Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila
anachokisema.
2.
Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo
jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
3.
Msomaji anatakiwa kuandika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili
kumasidia kukumbuka hapo baadae.
4.
Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha
kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia
kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.
Kusikiliza |
Kufupisha kwa Mdomo
Habari uliyoisikiliza
Ili
kuweza kufupisha kwa mdomo habari uliyoisikiliza yapo mambo ya kuzingatia.
Mambo hayo ni kubaini mawazo makuu yanayopaswa yajitokeze katika habari
iliyofupishwa, kupanga maelezo kwa usahihi katika usemaji, kuzingatia kichwa
cha habari ambacho kinapaswa kihusiane na ufupisho na wazo kuu na mwisho ni
kusema ufupisho kwa ufasaha na kwa lugha ambayo ni nzuri.
Zoezi
Fupisha
kwa mdomo habari uliyoisikiliza
UFAHAMU
WA KUSOMA
Ufahamu
wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari,
kitabu au gazeti.
Kusoma kwa Sauti kwa
kuzingatia Lafudhi ya Kiswahili
Kuna
vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:
1.
Uelewa wa msamiati na
2.
Uelewa wa matini
Ili
kuilelewa habari/matini ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika
katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka vilevile matini
yote hataeleweka.
Katika ufahamu wa
kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Kubaini mawazo
makuu;
msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatakiwa ajiulize, Je,
kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi?
Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa
habari hiyo.
2. Kuzingatia alama
za uakifishi;
msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia
kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji
anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
3. Kubaini maana ya
maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni
muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii
itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
4.
Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele
anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa
kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma
na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.
Kusoma |
Kujibu Maswali
kutokana na Habari uliyoisoma
Ili
kujibu maswali yanayotokana na habari uliyoisoma inatakiwa kuzingatia mambo
yafuatayo; kubaini mawazo makuu, kuzingatia alama za uandishi, kubaini maana ya
maneno na misemo mbalimbali na kutilia maanani vidokezo vya maana. Aidha mawazo
yanapaswa kuelekezwa katika jambo linalosomwa, kujiuliza maswali kadri
unavyosoma na kuandika ufupisho.
Kufupisha Habari
uliyoisoma
Ili
kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyosoma yapaswa kuzingatia yafuatayo:
kuisoma habari uliyopewa zaidi ya mara moja, kubainisha mawazo makuu, kuandika
ufupisho kwa lugha fasaha na yenye mtirirko mzuri wa hoja, kuhesabu idadi ya
maneno na kuhakikisha haizidi idadi inayotakiwa na kupitia habari ya mwanzo na
kisha ufupisho ili kuona kama taarifa muhimu haijaachwa au kusahaulika.
KUSOMA
KWA BURUDANI
Huu
ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa
aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida na vitabu tofauti na vile
vinavyotumika darasani. Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote
ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji
anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu nachokihitaji.
Ingawa
lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii
ni kwa sababu, magazeti, majarida na vitabu sambamba na kutuamia lugha sanifu
huelezea mambo mabalimbali yanayoihusu jamii.
Mambo ya Kuzingatia
katika Usomaji kwa Burudani
Msomaji
kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa
wa lugha na mambo mengine ya kijamaii yanayojadiliwa humo. Ni jambo zuri kwa
msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa
aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia
utaratibu w kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho
wa kila makala.
Utaratibu
unaopendekezwa katika kujipima na kujiwekea kumbukumbu ya usomaji wa burudani
ni kama ufuatao:
1.
Tarehe...
2.
Jina la kitabu/makala/gazeti....
3.
Mchapishaji......
4.
Mwaka/tarehe ya uchapishaji.....
5.
Ufupisho wa habari(yasizidi maneno 20)
6.
Fundisho/ujumbe mkuu ni.....
7.
Jambo lililokuvutia sana......
8.
Maoni kwa ujumla kama yapo....
Kusoma kwa burudani |
MATUMIZI
YA KAMUSI
Kamusi
ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa
jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna
ambayo wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika
karatasi au nakala tepe yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na
maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au
katika mfumo wowote wa kielekroniki.
Jinsi ya Kutumia
Kamusi
Maneno
yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno
yanayoanza na herufia, yote huwekwa chini ya herufiA. Maneno
yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa
kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano hapa chini
unavyoonyesha.
Mfano: ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno
yote yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya
tatu ni [b] na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti
maneno yenye [b] kabla ya yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni
mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague
litakaloorodheshwa mwanzo. Neno ‘jabali’ litaorodhewshwa kabla ya ‘jabiri’ kwa
kuwa [a] (herufi ya nne) ya ‘jabali’ hutangulia [i] ya ‘jabiri’ ambayo pia ni
herufi ya nne. Kisha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa
tunaangalia pia herufi ya nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya
‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa kuwa [h] hutangulia [i] basi ‘jadhibika’
huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na ‘jadi’.
Kwa
hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi
ya neno ulalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya
kwanza kuorodheshwa.
Neno
linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwa kidahizo. Kidahizo
huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana
ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo
n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwa kitomeo cha kamusi.
Kutafuta maana
unayoitaka
Neno
linaweza kuwa na maana moja au zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji
kamusi hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno
linapokuwa na maana zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi
aichague. Ili kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana
ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.
Mfano: kifungo
nm vi-
1.
kitu cha kufungia
2. kitu kinachotumiwa kufungia vazi
kama vile shati, gauni, suruali n.k
3.
adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda Fulani
Iwapo
mtumiaji aliona neno ‘kifungo’ kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha
miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha huu
itakuwa ni ile maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo
neno kifungo limetumika na wala sio maana ya 1 wala ya 2.
EmoticonEmoticon