FASIHI ANDISHI
Tamthiliya na Riwaya
ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani
ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari
mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile,
dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k
Nafasi ya Mhakiki
Uhakiki
ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo
uhakiki una dhima zifuatazo:
urahisi; Watunzi
wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo
mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi
kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi.
wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na kutunga
kazi iliyobora zaidi.
fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo yanayotokea katika
jamii.
ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi, Mhakaki ndiye anafafanua kazi ya fasihi
ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo. Kwa hiyo hapa mhakiki
anasaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi. Vilevile mtunzi huwaonyesha
watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi
kufanya kazi bora zaidi.
Hatua za Kufuata
wakati wa Kufanya Uhakiki
mtunzi huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao. Kwa kufanya hivyo
huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.
Kwanza ni kuisoma kazi ya fasihi; hapa mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya
fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.
Pili ni kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo
katika vipengele vya fani na maudhui.
Tatu ni kutoa tathimini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.
ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha
mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na hufuata utaratibu
fulani.
yapo ya aina mbili:
Mashairi ya Arudhi
ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa mashairi.
Arudhi/kanuni hizi ni pamoja na:
- Kugawika
kwa shairi katika beti - Beti
kuwa na idadi maalum ya mishororo. - Mishororo
ya ubeti kugawika katika vipande - Mishororo
kuwa na ulinganifu wa mizani - Shairi
kuwa na urari wa vina - Shairi
kuweza kuimbika / kuwa na mahadhi au mapigo. - Kuwepo
kwa kipokeo katika shairi - Kuwa
na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwala - hairi
kuwa na utoshelezo wa beti / kujisimamia kimaana.
hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiozingatia lazima
ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu huweza kuwa:
- Lugha
ya muhtasari - Lugha
yenye mahadhi - Lugha
ya kisanii iliyo na mafumbo na taswira - Mara
nyingine hugawika katika beti. - Mishororo
kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)
huwa na sifa maalum zinazoyatambulisha kama kazi ya kishairi, yawe ya kimapokeo
au kimapinduzi. Sifa
hizi ni kama vile:
- Mashairi
hutumia lugha ya mkato / muhtasari - Ni
sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundi - Huwa
na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi beti. - Hutumia
lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na jazanda. - Mashairi
huwa na sifa ya kuweza kuimbika hivyo shairi ni wimbo na wimbo ni shairi.
- Kupasha
ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvuto - Kuelimisha
na kuzindua jamii. - Kuendeleza
na kukuza kipawa cha utunzi. - Kuhifadhi
msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi. - Kuburudisha
hadhira na wasomaji. - Kuwasilisha
hisia za ndani za mtu na mawazo
Mashairi
- Soma
shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumla. - Soma
shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali na
kuchunguza maana ya kila mojawapo - Pitia
maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu yanayotarajiwa. - Soma
shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu
maswali. - Toa
majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririko.
Uchambuzi Wa Mashairi
1. Anwani/kichwa cha
shairi –
Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au sentensi moja. Anwani ni kidokezo
muhimu cha kinachozungumziwa katika shairi. Anwani huweza kuwa ya moja kwa
moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina
anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na maudhui au dhamira kwasentensi
isiyozidi maneno 6.
muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi. Kwa
mfano: malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k. Maudhui
hung’amuliwa kwa wepesi kutokana na kisa kilichomo katika shairi.
– Ni
lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni
ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi
katika shairi. Mfano: Baada ya kusoma shairi, unaweza kung’amua mtunzi
alitaka kusisitiza kauli kuwa uongozi mbaya
haufai, misitu ni uhai
n.k. Dhamira hutokana na mwelekeo wa mawazo ya mshairi au falsafa yake.
za lugha –
Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi zilizotumiwa na mshairi katika
shairi.
Mazda
/ ziada / zidi – kurefusha maneno; enda
kuwa enenda.
/ muhtasari – Ni kufupisha maneno; aliyefika
kuwa alofika.
– Mbinu ya kugeuza msamiati / maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika
kana kwamba ni ya Kiswahili.
vilevile huitwa ukopaji au uswahilishaji.
Taarifa Muhimu za
Mwandishi wa kila Kitabu
Mwandishi
wa fasihi ni mtu anaeweza kubuni kazi ya fasihi na kuiweka katika maandishi.
Unaposoma kazi za fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi wa kazi
hiyo, ambazo ni jina, kwa sababu kila utakapokua unajibu swali ni lazima utaje
jina la mwandishi wa kitabu. Falsafa na utamaduni kujua msimamo wake, na muundo
kujua mpangilio wa matukio, mtindo kujua upekee wake na matumizi ya lugha.
2 Comments
uko vizuri kiongozi
Mbona kama hazjaisha hiv