Join Our Groups
TOPIC 2: AINA ZA MANENO
Katika
lugha ya Kiswahili kuna angalau aina nane za maneno ambazo wataalamu wengi wa
lugha wanakubaliana hivyo. Katika mada hii utaweza kujifunza na kubainisha aina
zote nane za maneno na jinsi zinvyotumika katika sentensi. Utaweza pia
kujifunza namna ya kutofautisha aina za maneno ambazo zimeleta ubishi miongoni
mwa wataalamu wengi hususani katika Viunganishi na Vihusishi.
Aina Saba za
Maneno ya Kiswahili
Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:
Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili ni pamoja na hizi zifuatazo:
Aina Nomino (N)
Viwakilishi
(W)
Vitenzi (T)
Vivumishi (V)
Vielezi (E)
Viunganishi
(U)
Vihusishi (H)
Vihisishi (I)
1. NOMINO (N)
Nomino
ni maneno yanayotaja vitu, watu, na hali kadhalika. Kuna aina mbali mbali za
maneno ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo:
1.
Nomino za
pekee
Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino
mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote.
Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito,
milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata
kama nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
2.
Nomino za
kawaida
Hizi
kwa jina jingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi wazi wazi
vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi
hatambuliwi. Haituambii kama ni Bahati, Bite ama Neema. Ikiwa ni mlima
hautambuliwi kama ni Meru , Kilimanjaro au Evarest, yaani hutaja vitu bila
kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee.Hizi zinapoandikwa si
lazima zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au
zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano
huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi
kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
3.
Nomino za
mguso
Nomino
za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na mwanadamu kupitia milango ya
hisia kama macho, mapua, masikio vidole na ulimi- yaani vitu vinavyoweza
kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
4.
Nomino za
jamii
Hizi
ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino
zinazotaja umla ya vitu vingi. Mfano; jozi ya viatu, umati wa watu, bustani ya
maua, bunga ya wanyama
5.
Nomiono
dhahania:
Kundi
hili la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa kuhesabika kuziainisha. Hapa
tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu vinavyohesabika kwa upande
mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande mwengine. Nomino ya vitu
vinavyohesabikavitanda, nyumba,vikombe vitabu na kadhalika.Zile zisizohesabika
hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na haviwezi kugawika, kwa mfano maji,
mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta. Aghalabu nomino hizo huwa sawa katika
umoja na wingi.
6.
Nomino za
kitenzi jina:
Hizi
ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha
unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe
nomino.
2. VIVUMISHI (V)
Vivumishi
ni maneno yanayoelezea zaidi juu ya nomino, aghalabu vivumishi hutanguliwa na
nomino. Kuna aina kadhaa za vivumushi, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi
vifuatavyo.
Vivumishi
vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo
1.
Vivumishi
vya sifa. Hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi
huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile.
2.
Vivumishi
vya idadi. Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya
nomino. Kuna vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi
ya nomino hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
3.
Vivumishi
vya idadi ambavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani
katika orodha.
4.
Vivumishi
vya kumiliki: Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina
milikiwa na mtu au kitu kingine.
5.
Vivumishi
Vioneshi. Vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu
kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi{h}kwa vitu vilivyopo karibu na
mzizi{le}kwa vitu vilivyo mbali.
6.
Vivumishi
vya kuuliza: Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza
habari zake. Hujibu swali “gani? ipi? ngapi?”
7.
Vivumishi
vya A- unganifu: Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa
kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi
ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali.Vivumishivya aina hii hutumika kuleta
dhana za–Umilikaji, - Nafasi katika orodha.
8.
Vivumishi
vya jina kwa jina: Hizi ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo
hutumika kufafanua nomino
9.
Vivumishi
vya pekee. Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila
kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake
wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha.
Mizizi
vivumishi hivi niote, o-ote, -enye, -enyewe, -ingine, -ingineo.
-
ote:Huonyesha ujumla wa kitu au vitu
-
o-ote:Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”
–
enye:Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino
fulani.
-
enyewe:Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.
–
ingine:Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’
kitu fulani
–
ingineo:Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.
3. VIELEZI (E)
Vielezi
ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu
kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi.
Aina za vielezi
1.
Vielezi vya
Mahali. Vielezi vya mahali hutoa habari kuhusu mahali ambapo kitendo
kilifanyika. Aghalabu vielezi hivi huundwa kwa kutumia jina la mahali au kwa
kuongeza kiungo -NI mwishoni mwa neno linaloashiria mahali.Kwa mfano:nyumbani,
kazini, shuleni
Example
1. Mtoto
huyo hajatulia nyumbani tangu alipotoka Mombasa.
2. Msipitie sokoni mkienda kanisani.
2.
Vielezi vya
Wakati. Huelezea zaidi kuhusu wakati kitendo kinapofanyika; kwa
mfano: jioni, jana, asubuhi, saa saba, mwaka juzi.
Example
1. Mzee
Kasorogani amesema kwamba ataoga mwaka ujao
2. Musa alilazimishwa kuchimba mtaro saa sita usiku
3. Kisaka na Musa watakutana kesho
3.
Vielezi vya
Idadi. Vielezi vya idadi hutulezea kitendo kilifanyika mara ngapi.
a)
Idadi Kamili: Vielezi vya Idadi Kamili hutaja idadi kamili ya mara ngapi
kitendo kilifanyika. Kwa mfano:mara mbili, siku mbili kwa juma, mara kumi
Example
1
1.
Gibi alimzaba kofi mara tatu na kisha akakimbia
2. Daktari
alimwagiza mama huyo achukue dawa mara tatu kwa siku na arudi hospitalini siku
mbili kwa mwezi
b)
Idadi Isiyodhihirika: Vielezi vya Idadi Isiyodhirika huelezea kiasi ambacho
kitendo kilifanyika bila kutaja kiasi kamili kwa mfano:chache, nyingi, kadhaa,
kidogo, wastani.
Example
2
Mwizi
wa kuku alipigwa mara kadhaa kabla ya kuokolewa na polisi.
Yeye
hunipigia simu mara kwa mara.
4.
Vielezi vya
Namna au Jinsi. Vielezivya namna hii huonyesha jinsi au namna
kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
5.
Vielezi vya
Namna Halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi
yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno.
6.
Vielezi vya
Namna Mfanano. Hivi ni vieleziambavyo hutumika kufananisha vitendo
na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi(ki-) au
kiambishi(vi-).Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano.
Mfano; Ulifanyavizurikumsaidia
mwanangu.
7.
Vielezi vya
Namna Vikariri. Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa
kurudiarudia neno moja mara mbili.
8.
Vielezi vya
Namna Hali. Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka
kimetendeka katika hali gani.
9.
Vielezi vya
Namna ala/kitumizi. Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo
hutumika kutendea kitendo
10.
Vielezi vya
Namna Viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa
kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au
kutokea.
11.
Vielezi vya
Wakati. Vielezivya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa
kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi{po}
4. VITENZI
Kitenzi
ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu
lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo Kitenzi cha Kiswahili
huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti
Aina za Vitenzi
1.
Vitenzi
vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu
cha sentensi.
2.
Vitenzi
visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa
taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi visaidizi daima hutumika
na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati.
3.
Vitenzi
vishirikishi: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui
viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina
mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi“ni” cha uyakinishina kitenzi shirikishi
“si” si cha ukanushi.
4.
Vitenzi
vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya
nafsi, njeo na hata hali. Kwa mfano;ndiye, ndio, ndipo.
Kazi za Kitenzi Kikuu
1.
Kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
2.
Kuonyesha wakati tendo linapotendeka
3.
Kuonyesha hali ya tendo
4. Kuonyesha nafsi
5.
Kuonyesha kauli mbali mbali za tendo
6. Kuonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
Kazi za Kitenzi
Kishirikishi
1.
Kushirikisha vipashio vingine katika sentensi
2. Kuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu
fullani.
3.
Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.
4. Kuonyesha sifa za mtu.
5.
Kuonyesha umoja wa vitu au watu
6. Kuonyesha mahali
7.
Kuonyesha msisitizo
8.
Kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
Aina za Wakati Katika
Kitenzi
- Wakati uliopita
- Wakati uliopo
- Wakati ujao
Hali mbalimbali
za kitenzi
-
Hali ya masharti
- Hali ya
kuendelea kwa tendo
- Hali ya kutarajia, kuamuru na kuhimiza
5. VIWAKILISHI
Viwakilishi
ni aina ya neno linaloweza kutumika badala ya jina/nomino .
Aina za Viwakilishi
1.
Viwakilishi
vioneshi au viwakilishi vya kuonesha. Viwakilishi vionyeshi hutumika
badala ya nomino kwa kutumia kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja. Kwa
mfano; huyu, yule, hapo, kule, humo. Huyu si mwenzetu kabisa; kule hakufai kwenda
watoto.
2.
Viwakilishi
vya nafsi: Kwa mfano: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao
3.
Viwakilishi
vya kuuliza/viwakilishi viulizi. Ambavyo huashiriwa na mofu
/kiambishi{-pi}ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina
husika. Kwa mfano, Wangapi wameondoka? Kipi kimekosewa?
4.
Viwakilishi
vya urejeshi. Ambavyo vinajengwa na shinaambapamoja na vipande
vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, kon.k ambavyo vinachaguliwa
kulingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo. Mfano; aliyeondoko hatapewa
chake.
5.
Viwakilishi
vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo
huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
6.
Viwakilishi
vya pekee/vimilikishi. Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee
kuwakilisha nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
Mfano; '-angu, -ako, -ake, -etu, -enu, -ao '. kwangu haingii megini, chako
haikna thamani.
7.
Viwakilishi
vya A-Unganifu. Viwakilishi hivi huundwa kwa kihusishi
chaA-unganifukusimamia nomino iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika
orodha au nomino ya aina fulani. Kihusishi a-unganifu huandamana na nomino
kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino. Mfano;ya
kwakeyamemshinda,vya wazeehaviguswi.
8.
Viwakilishi
vya sifa: Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino
katika setensi. Kwa mfano -eupe, -janja, -tamu
7.
Viwakilishi
vya Idadi. Idadi Kamili- hutumia namba kuelezea idadi ya nomino.
'saba, mmoja, ishirini' -Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi
yake. Idadi Isiyodhihirika- huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja
idadi kamili: 'chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani'
6.
VIUNGANISHI
Ni
maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai,
kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi
vyenye hadhi sawa kisarufi.
Aina za Viunganishi
1.
Viunganishi
huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati
ya vipashio vinavyoungwa.Viunganishi huru hujumuisha:
2.
Viunganishi
nyongeza/vya kuongeza, kama vile, na, pia, pamoja. Baba na mwanae
wanacheza mpira, Alichukua chakula chote pamoja na akiba iliyokuwepo.
3.
Viunganishi
vya sababu/visababishi, mfano, kwa sababu, kwa kuwa, kwa vile,
madhali, ili. Alimsogelea karibu ila ambusu, Atatumikia kifungo madhali
amebainika kuwa na hatia.
4.
Viunganishi
vya uteuzi/chaguo. Mfano; au, Naweza kwenda nyumani au shuleni.
5.
Viunganishi
vya kutofautisha/vya kinyume:ila, lakini, kinyume na, japokuwa,
ingawa, ilihali. Mfano; Mkumbatie lakini usimbusu.
6.
Viunganishi
vya wakati. Wakati mfano; Mwalimu aliuliza swali wakati yeye
amesinzia.
7.
Viunganishi
vya masharti; ikiwa, iwapo, hadi. Mfano; utaruhusiwa kuingia hapa
ikiwa umevaa mavazi yanaostahili.
8.
Viunganishi
vihusishi; miongoni mwa, kati ya; mfano: Jane alikuwa miongoni mwa
washindi kumbi bora kitaifa.
9.
Viunganishi
tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi
tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja
huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -po-, -cho-, -o- Nili-po-amka…,
Ali-cho-mwelez…, alizo-o-neshwa…n.k
7.
VIHUSISHI
Ni
maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jingine.
Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno
mengine.
Mambo yanayoweza
Kuonyeshwa na Vihusishi
1.
Huonyesha uhusiano wa kiwakati; Mfano, ni vizuri kupiga mswakibaada yachakula.
2. Huonyesha uhusiano wa mahali: mfano, Ninaishikaribu nakwa Mtogole
3.
Huonyesha uhusiano wa kulinganisha: Amekulazaidi yauwezo wake.
4. Huonyesha uhusiano wa umilikaji: Usiguse hicho kitabu nicha kwangu
5.
Huonyesha uhusiano wa sababu/kiini: nimerudi kwaajili yakuonana na mkuu wa
shule.
Aina za Vihusishi
1.
Vihusishi vya wakati
2. Vihusishi vya mahali
3.
Vihusishi vya vya kulinganisha
4. Vihusishi vya sababu
5.
Vihusishi vya ala/kifaa mfano; kwa
6. Vihusishi vimilikishi
7.
vihusishi vya namna; Kichwacha mviringo
8. Vihusishi ‘na’ cha mtenda mfano, amepigwana Juma.
Matumizi ya
kihusishi “kwa”
1.
Huonyesha mahali au upande: Mfano, amekwenda kwa mjomba wake.
2.
Huonyesha sababu au kisababishi cha jambo: mfano; ninaishi kwa ajili yako.
3.
Huonyesha wakati: mfano; sina nafasi kwa sasa.
4.
Huonyesha sehemu fulani ya kitu kikubwa, mfano: Mpira umekwisha wakiwa
wamefungana nne kwa tatu.
5.
Huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka: Mfano; alimvuta kwa nguvu sana ndo
maana limevunjika.
8.
VIHISISHI/VIINGIZI
Ni
maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
Vihusishi vinaweza
kugawanywa katika makundi yafuatayo:
1. Vihisishi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
2. Vihisishi vya furaha
3. Vihisishi vya huzuni
4. Vihisishi vya mshituko
5. Vihisishi vya mshangao
Vihisishi vya
maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio
1.
Vihisishi vya maadili
2. Vihisishi vya mwiitiko
3.
Vihisishi vya ombi
4. Vihisishi vya bezo
5.
Vihisishi vya kutakia heri
6.
Vihisishi vya kukiri afya/jambo
7.
Vihisishi vya kiapo
8. Vihisishi vya salamu
Matumizi ya Aina
za Maneno katika Tungo
Aina
za maneno hutumika katika tungo kwa kutegemeana na lengo la msemaji. Kwa mfano
kama lengo la msemaji ni kuonesha aina fulani ya hisia atatumia vihisishi
katika tungo yake. Vilevile kama msemaji anahitaji kueleza kuhusu namna nomino
inavyotenda, ilivyotendewa au inavyotendwa, atatumia kitenzi.
MATUMIZI YA
KAMUSI
Kamusi
ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa
jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna
ambayo wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika
karatasi au nakala tepe yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na
maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au
katika mfumo wowote wa kielekroniki. Kamusi
huweza kuwa ya lugha moja, yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo yake yakiwa
katika lugha moja
Example
1
Mfano:
chatu ni nyoka mkubwa na mnene
Kamusi
nyingine huwa za lugha mbili yaani orodha ya maneno ipo katika lugha moja na
maelezo ya maana ya maneno hayo yapo katika lugha nyingine.
Example
2
chatu,
n python
Kamusi
ni hazina ya lugha inayohusika, kwani tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa
na orodha ya maneno mbali mbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile
pamoja na maana zake. Japokuwa wingi wa maneno hutegemea ukubwa wa kamusi,
kitabu hiki kina manufaa makubwa kwa mtumiaji wake kwani humpatia msamiati
asioufahamu pamoja na maana zake au humpatia maana zaidi ya maneno
anayoyafahamu.
Awali
kamusi zilipoanza kutungwa zilikuwa ni orodha ya maneno magumu pamoja na maana
zake. Kamusi za siku hizi huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongoni mwa taarifa
ambazo kamusi huwa nazo ni:
1.
Tahajia za maneno mfano. Tasinifu Vs Tasnifu, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs
Kura, -ingine vs -engine
2.
Matamshi
3.
Sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno kama vile maumbo ya wingi
wa nomino, vinyambuo vya neno kama vile chezesha, chezeka, chezea, mchezo,
mchezajin.k ambavyo vinatokana na kitenzi cheza
4.
Maana
5.
Etimolojia ya neno (asili ya neno husika)
6.
Matumizi ya neno
Jinsi ya Kutumia
Kamusi
Maneno
yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno
yanayoanza na herufi a, yote huwekwa chini ya herufi A. Maneno yanayoanza na
herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi
ya pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano hapa chini unavyoonyesha.
Example
1
Mfano:ja,
jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno
yote yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya
tatu ni [b] na [d]. Kwa kuwa [b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti
maneno yenye [b] kabla ya yale yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni mawili
itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa
mwanzo. Neno ‘jabali’ litaorodhewshwa kabla ya ‘jabiri’ kwa kuwa [a] (herufi ya
nne) ya ‘jabali’ hutangulia [i] ya ‘jabiri’ ambayo pia ni herufi ya nne. Kisha
tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya
nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya ‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa
kuwa [h] hutangulia [i] basi ‘jadhibika’ huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na
‘jadi’.
Kwa
hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi
ya neno unalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya
kwanza kuorodheshwa.
Neno
linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwakidahizo.Kidahizo
huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana
ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo
n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwakitomeo cha kamusi.
Example
2
Kitomeo
cha kamusi
Dhabihu
(kidahizo) nm (kategoria ya neno)
mahali pa kuchinjia wanyama (maana ya neno).
Taarifa
Ziingizwazo katika Kamusi
Fafanua
taarifa ziingizwazo katika kamusi
Maana
za maneno
Kwa
mfano: Dhabihu
nm mahali pa kuchinjia wanyama.
Kategoria za Maneno
Kategoria
za maneno kama vile kielezi (ele), kitenzi (kt), kivumishi (kv), nomino (nm),
kihisishi.
Mifano ya Matumizi
Kwa
mfano, Waiziraeli huwapeleka koondo wao kwenye dhabihu kwa ajili ya ondoleo la
dhambi. Lengo la kutoa mifano ni kumsaidia msomaji asiye fahamu vyema neno husika
aelewe jinsi neno hilo linavyotumika.
Uingizaji wa
nomino
Nomino
nyingi katika lugha ya kiswaili zina maumbo ya umoja na wingi.
Mfano:
dume
nmma-
mkopo;
nm mi-
Viambishi
ambatishi huwekwa kando ya nomino kuashiria umbo la wingi la nomino.
Ngeli
za nomino
Mfano:
mkopo
nmmi- [u-/i-]
Kutafuta maana
unayoitaka
Neno
linaweza kuwa na maana moja au zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji
kamusi hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno
linapokuwa na maana zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi
aichague. Ili kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana
ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa.
Mfano:
kifungo
nm vi-
1.
Kitu cha kufungia
2.
Kitu kinachotumiwa kufungia vazi kama vile shati, gauni, suruali n.k
3.
Adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda fulani
Iwapo
mtumiaji aliona neno ‘kifungo’ kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha
miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha huu
itakuwa ni ile maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo
neno kifungo limetumika na wala sio maana ya 1 wala ya 2.
EmoticonEmoticon