Join Our Groups
TOPIC 3: FASIHI KWA
UJUMLA
Fasihi
ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu binadamu matatizo yake,
ndoto zake, matumaini yake, migogoro yake na jinsi anavyoingiliana na mazingira
yake. (Wamitila, 2004). Fasili hii imejaribu kufafanua vizuri kile ambacho
fasihi inajihusisha nacho, kimsingi fasihi inajihusisha na wanadamu. Vitu vya
msingi tunavyoviona katika fasili hii ni kwamba fasihi ni sanaa, na fasihi
inatumia lugha lakini zaidi fasihi inajihusisha na wanadamu.
Dhima za Fasihi katika
Jamii
Dhima
za fasihi katika jamii ni pamoja na hizi zifuatazo:
1. Kuburudisha jamii:Pamoja na mambo mengine fasihi
inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa
na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia
nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika.
2. Kuelimisha. Fasihi hutumika kama nyenzo ya
kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo
mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa
kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika.
3. Kuonya jamii. Fasihi ina jukumu la kuhakikisha
wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi
wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika
jamii.
4. Kuunganisha jamii. Fasihi huleta watu katika jamii.
Watu huunganishwa kupitia kazi mbalimbali za kifasihi, kwa mfano, kupitia
nyimbo, miviga, vichekesho na kadhalika.
5. Kukuza lugha.Fasihi hutumia lugha kufikisha
ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo
kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji. Mtu anaposoma au
kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia fasihi yenyewe
inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na waandishi wa
fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.
6. Kuhifadhi mila,
tamaduni na itikadi za jamii. Kupitia fasihi simulizi, tamaduni
na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau
na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.
7. Kukuza uwezo wa
kufikiri.
Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho.
Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.
AINA
ZA FASIHI
Kuna
tanzu mbili za fasihi, ambazo ni fasihi andishi na fasihi simulizi.
1. FASIHI
SIMULIZI
Fasihi
Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa
kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.
Sifa za Fasihi
Simulizi
1.
Hupitishwa kwa njia ya mdomo
2.
Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au
wahusika.
3.
Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
4.
Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
5.
Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa
sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
6.
Aghalabu huwa na funzo fulani
Dhima za Fasihi
Simulizi
1.
Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
2.
Kunasihi - kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii.
3.
Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
4.
Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika
fasihi simulizi kama vile nyimbo.
5.
Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
6.
Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
8.
Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
9.
Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.
10.
Fasihi simulizi ni chombo cha mawasiliano hususani kupitia ngomezi.
2.
FASIHI
ANDISHI
Fasihi
Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno ya maandishi kupitisha ujumbe
kwa hadhira.
Kuna tanzu kuu nne za
Fasihi Andishi:
1. Hadithi Fupi – Hii ni kazi ya fasihi andishi
yenye kisa kimoja na mhusika mkuu mmoja na maudhui yake sio changamani.
2. Riwaya –Ni kazi ya fasihi andishi yenye
wahusika wengi na muundo changamani ni ndefu na maudhui yake ni mapana.
3. Tamthilia- ni kazi ya kisanaa yenye muundo wa
kiugizikaji inayowasilishwa katika maandishi.
4. Mashairi - mashairi yakiwa yamechapishwa pia
hutambulika kama fasihi andishi.
1.
Hupitishwa kwa njia ya maandishi
2.
Ni mali ya mtu binafsi
3.
Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
4.
Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika uwasilishaji wake.
Dhima za Fasihi
Andishi
1.
Kukuza lugha
2.
Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
3.
Kuburudisha
4.
Kuelimisha
5.
Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
6.
Kuonya, kuelekeza, kunasihi
Tofauti kati ya Fasihi
Simulizi na Fasihi Andishi
Zifuatazo
ni tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi kama zilivyobainishwa
katika jedwali hapa chini:
That's great thanks
ReplyDelete