Join Our Groups
TOPIC 4: FASIHI SIMULIZI
Fasihi
simulizi ni moja kati ya tanzu za fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka
kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo. Katika mada hii utajifunza na
kisha utaweza kubainisha tanzu na vipera vya fasihi simulizi pamoja na
ufafanuzi wake. Na pia utaweza kutofautisha kati ya kipera na kipera au kati ya
utanzu na utanzu.
Tanzu za Fasihi
Simulizi
Fasihi
Simulizi ni kazi ya fasihi inayohifadhiwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja
hadi kingine kwa njia ya mdomo kama vile; hadithi, ngoma na vitendawili.
Tanzu
za Fasihi Simulizi ni pamoja na hizi zifuatazo:
- Masimulizi/hadithi
- Semi
- Ushairi
- Mazungumzo
- Maigizo
- Ngomezi
Vipera vya Tanzu za
Fasihi Simulizi
1. SIMULIZI/
HADITHI
Masimulizi
ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Ni masimulizi ambayo yanatumia lugha
ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi
hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zipo hadithi
ambazo ni za kubuni na zingine za kihistoria. Baadhi ya vipera vya utanzu huu
ni:
NGANO
1. Istiara – hadithi ambayo maana yake ya wazi
inawakilisha maana nyingine iliyofichika. Yaani hadithi nzima ni kama sitiari.
2. Mbazi- hadithi fupi yenye mafunzo
itolewayo kama kielelezo wakati wa maongezi au wa kumkanya mtu
3. Kisa- hadithi fupi ya kufurahisha kuhusu
tukio la kweli.
VISAKALE
Masimulizi
ya kimapokeo juu ya wahenga au mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya
chuku na historia. Kwa mfano hadithi za Liyongo
MAPISI
Maelezo
ya historia bila kutia mambo ya kubuni.
SOGA
Ni
hadithi ndogo ndogo zinazohusisha utani na ucheshi kwa kiasi fulani. Hizi ni
hadithi ambazo hutambwa katika mtiririko wa matukio ambao huzua kicheko. Soga
hudhamiria kuchekesha na pia kukejeli.
TARIHI
Hizi
ni hadithi ambazo husimulia au zimejengwa kwenye matukio ya kihistoria.
Inawezekana matukio yanayosimuliwa yakawa ya kweli, yaani yalipata kutokea
kihistoria. Hadithi hizi hutokea zaidi katika maandishi.
VISASILI
Ni
utanzu unaofungamana na imani za dini na mizungu ya jamii. Hizi ni hadithi za
kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya
ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya
maisha yao. Mara nyingi hadithi hizi huaminiwa kuwa ni kweli tupu, na hutumika
kuelezea au kuhalalisha baadhi ya mila na madhehebu ya jamii inayohusika.
2. USHAIRI
Huu
ni utanzu wa fasihi simulizi unaowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au
ughani badala ya usemaji wa kawaida. Katika utanzu huu kuna vipera viwili
ambavyo ni nyimbo na maghani.
NYIMBO
Nyimbo
ni kila kinachoimbwa. Kipera hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo
ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi,
mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa,
nyimbo za watoto na nyimbo za kazi.
1. Tumbuizo:
hizi
ni nyimbo za furaha ziimbwazo kuwafurahisha watu kwenye matukio mbalimbali kama
vile ngomani au harusini. Bembea; hizi ni nyimbo za kubembeleza watoto. Kigezo
kilichotumika hapa ni kigezo cha kidhima ambapo hulenga kubembeleza watoto.
2. Kongozi:
hizi
ni nyimbo za kuaga mwaka.
3. Nyimbo za dini:
hizi ni nyimbo
zinazoimbwa kwa lengo la kumsifu Mungu au miungu.
4. Wawe:
hizi
ni nyimbo za kilimo; huuimbwa wakati wa kulima.
5. Tenzi:
hizi
ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au mawaidha.
6. Tendi:
hizi
ni nyimbo ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa, wahusika wa tendi ni
watu wenye historia za matendo ya kishujaa.
7. Mbolezi:
hizi ni nyimbo za
kilio au maombolezo.
8. Kimai:
hizi
ni nyimbo zihusuzo shughuli za baharini.
9. Nyiso:
hizi
ni nyimbo za jandoni.
10. Nyimbo za vita:
hizi
ni nyimbo ziimbwazo na askari wakati wa vita.
11. Nyimbo za watoto:
hizi ni nyimbo
waimbazo watoto wakati wa michezo yao.
12. Nyimbo za
uwindaji: hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na
makundi ya wawindaji wakati wa shughuli au sherehe zao.
13. Nyimbo za Taifa: hizi ni nyimbo za kusifia Taifa au kabila.
14. Nyimbo za kazi: hizi ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali kama
vile, kulima, kutwanga, kusuka, uvuvi, uashi, useremala na kadhalika
MAGHANI
Maghani
ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au
maneno badala ya kuimbwa. Kipera hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida,sifo na maghani masimulizi.
1. Maghani ya kawaida
ni
kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile
ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika
namna ya uwasilishwaji wake.
2. Sifo: hizi ni tungo za kusifu ambazo
husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli.
Sifo huwa na tanzu muhimu kama vile vivugo
(majigambo), pembe zinatondozi.
a) Kivugo:
hili
ni ghani la kujisifia, hutungwa na kughanwa na muhusika mwenyewe.
b) Tondozi:
hizi
ni tungo za kusifu watu, wanyama au vitu.
3. Ghani masimulizi:
hizi
ni ghani ambazo hutambwa ili kusimulia hadithi, historia au tukio fulani. Ghani
masimulizi ina vipera vinne ambavyo ni rara, ngano, sifo na tendi.
a) Rara ni hadithi fupi nyepesi ya kishairi
yenye visa vya kusisimua; rara huimbwa au kughanwa ikiambatana na ala za
muziki.
b) Ngano:
hizi
ni hadithi za mapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika
kuelezea au kuonya kuhusu maisha.Ngano huwa ghani masimulizi inapowasilishwa
pamoja na ala ya muziki.
c) Sifo:
hizi
ni tungo za kusifu: sifo huwa ghani masimulizi inapoingiza muziki katika
utondozi wake, lugha iliyotumika ni lugha ya kishairi.
d) Tendi:
hizi
ni ghani ndefu za masimulizi juu ya matendo ya mashujaa yenye uzito kijamii au
kitaifa.
3. SEMI
Semi
ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zenye kubeba maana au mafunzo muhimu ya
kijamii. Baadhi ya tanzu katika kundi hili ni:
1. Methali: Methali ni semi fupi fupi zenye
kueleza kwa muhtasari fikra au mafunzo, mazito yaliyotokana na uzoefu wa
kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na
mafumbo. Methali nyingi huwa na muundo wenye sehemu mbili. Sehemu ya kwanza huanzisha
wazo fulani, na sehemu ya pili hulikanusha au kulikaamilsha wazo hilo. Kwa
mfano; mwenda pole hajikwai, aliye juu mngoje chini.
2. Vitendawili: Ni usemi uliofumbwa ambao hutolewa
kwa hadhira ili iufumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii
hiyo, na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki, mbali na kuwachemsha
bongo zao. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha
na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile.
3. Misimu: Ni semi za muda na mahali maalum
ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya
kutosha katika jamii huweza hatimaye kuingia katika kundi la methali za jamii
hiyo.
4. Mafumbo: Ni semi za maonyo au mawaidha
ambazo maana zake za ndani zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha
na hadhira maalum, hivyo ni tofauti na methali au vitendawili ambavyo ni semi
za kimapokeo.
4. Lakabu: Haya ni majina ya kupanga ambayo
baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba,
kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni maneno au mafungu ya maneno yenye
maana iliyofumbwa. Mara nyingi majina haya huwa ni sitiari. Baadhi ya majina
haya humsifia mhusika, lakini mengine humkosoa au hata kumdhalilisha; Mifano:
simba wa yuda- Hali Selassie, Baba wa taifa – Mwl Nyerere.
4. MAIGIZO
Maigizo
ni mchezo ambao hutumia watendaji wa kuiga tabia na matendo ya watu au viumbe
wengine ili kuburudisha na kutoa ujumbe fulani kwa hadhira.
UHAKIKI WA KAZI ZA
FASIHI SIMULIZI
Umuhimu wa Uhakiki wa
Kazi za Fasihi Simulizi
Umuhimu
wa uhakiki wa kazi za fasihi simulizi ni kubaini ubora wa kazi za fasihi
simulizi, kubaini vipengele mbalimbali vya fani na maudhui, kupima namna kazi
inavyoambatana na mazingira inamotokea, kupima kufaa na kutokufaa kwa fasihi
simulizi, kubaini ukweli wa mambo yanayoelezwa, kuangalia uhalisi wa watu na
mazingira katika jamii na kubaini umuhimu wa kazi ya fasihi katika jamii
husika.
Vigezo vya Uhakiki wa
Kazi za Fasihi Simulizi
Uhakiki
wa kazi ya fasihi huzingatia vigezo viwili ambavyo vimegawanyika katika
vipengele mbalimbali. Vigezo hivyo ni fani na maudhui. Katika kigezo cha fani
mhakiki atazingatia muundo, mtindo, matumizi ya lugha, wahusika na mandhari
wakati katika kigezo cha maudhui mhakiki atazingatia dhamira, migogoro,
falsafa, msimamo na ujumbe.
Uhakiki wa Hadithi
Uhakiki
wa hadithi kama ilivyo katika kazi nyingine za fasihi simulizi umejikita katika
kuchunguza vipengele mbalimbali vya fani na maudhui. Vipengele vya fani ni
muundo, mtindo, wahusika, mandhari na matumizi ya lugha. Aidha kwa upande wa
maudhui, vipengele vyake ni dhamira, migogoro, falsafa, ujumbe na msimamo.
Matumizi ya Semi
katika Hadithi
Uhakiki
wa semi katika fasihi umejikita kuangalia usahihi wa matumizi ya vipengele
mbalimbali vya lugha katika kazi ya fasihi inayohusika. Vipengele hivyo ni
misemo, nahau na mafumbo. Vilevile uhakiki wa semi umejikita katika kuchunguza
namna lugha ilivyofuzu kigezo cha kwenda na wakati.
Dowload
返信削除Nakubali sana uchambuzi wenu wa notisi..
返信削除