Join Our Groups
TOPIC
3: MAENDELEO YA KISWAHILI
ASILI YA KISWAHILI
Neno
asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Kutokana na fasili
hii tunaona kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika
lugha au linaweza kuanzishwa.
Hivyo
basi asili ya lugha ya Kiswahili bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu
mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko la lugha ya kiswahili. Wapo
wanaokinasibisha kiswahili na kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati na dini
ya kiislamu. Wengine wanashikilia msimamo kuwa kiswahili ni kibantu kwa kutumia
hoja za kiisimu na kihistoria. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na uchotara
baadhi yao wanaoshikilia msimamo huu ni Freeman Grenville na Homo Sasson
Kuna
nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea asili ya Kiswahili, miongoni mwa hizo
ni pamoja na hizi zifuatazo:
Kiswahili ni Kiarabu
Hapa
Kiswahili kimefasiliwa kuwa asili yake ni kiarabu, wanaoshikilia mtazamo huu
wanahoji kwamba katika lugha ya Kiswahili kuna maneno mengi ya Kiarabu. Pia
wanaeleza kuwa asili ya Kiswahili ni pwani na kwa kuwa wenyeji wa pwani ni
Waislamu na kwa kuwa uislamu uliletwa na Waarabu basi hii lugha ya pwani nayo
itakuwa imeletwa na Waarabu. Vigezo hivyo vyote vina udhaifu mkubwa kwa sababu
havikukitwa katika misingi ya kitaalamu ya uainishaji lugha.
Kiswahili ni Lugha
Chotara
Mtazamo
huu umezua ubishi mkubwa kwani hata baadhi ya wazawa wamejinasibisha na uarabu
na ushirazi. Wanaofasili Kiswahili kama lugha chotara wanadai kuwa Kiswahili
kimetokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kibantu. Hivyo
Waswahili ni watu waliotokana na wanaume wa Kiarabu na wanawake wa Kibantu.
Kiswahili ni Lugha ya
Vizalia
Waumini
wa mtazamo huu wanadai kuwa Kiswahili kilianza kama pijini ya Kiarabu na baadae
kukomaa na kuwa kreoli. Pijini ni lugha ambayo imetokana na mchanganyiko wa
lugha mbili tofauti yaani Kiarabu na lugha za Kibantu. Na kreoli ni lugha
inayozungumzwa na watoto waliozaliwa na baba Mwarabu na mama Mbantu.
Kiswahili ni Kikongo
Nadharia
hii inafafanua kuwa lugha ya Kiswahili ilianzia huko Kongo na kusambaa katika
pwani ya Afika Mashariki. Wabatu walipofika Afrika Mashariki waliingia kwa
makundi na katika nyakati mbalibali. Makundi hayo yalianza kujigawa na
kutawanyika, matokeo ya kugawanyika huko ni kutokea kwa makundi mbalimbali ya
wabantu. Inasadikika kuwa baadhi ya Wabantu walifanya maskani yao ya kudumu
katika mabonde ya kaskazini mwa mto tana. Kikundi hiki cha wabantu ndicho
inasadikiwa kuwa chimbuko la Kiswahili
Kiswahili ni Kibantu
Mtazamo
huu ni ule unaoamini kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ambapo lugha za Kibantu
zilikuwepo hata kabla ya majilio ya wageni kutoka Ajemi, Arabuni, India, China
na kwingineko. Katika mtazamo huu lugha ya Kiswahili inaingizwa katika kundi la
lugha za Kibantu. Ama kwa hakika mtazamo huu ulipata mashiko sana kuanzia karne
ya ishirini, ulishadidiwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na weledi
wa isimu, historia, akiolojia na ethnografia. Wanaisimu waliothibitisha kuwa
Kiswahili ni lugha ya Kibantu ni pamoja na Bleek (1862), Meinholf. C (1932),
Malcom Guthrie (1967, 1970, 1971), Doke (1935, 1945) na wengineo. Vigezo
vilivyotumika kufafanua kuwa Kiswahili ni kibantu ni pamoja na:
- Msamiati
-
Mofolojia
-
Mfumo wa sauti
-
Mfumo wa toni
- Mfumo
wa ngeli
- Mpangilio
wa maneno
Ubantu wa Kiswahili:
Kigezo cha Kiisimu
Kigezo
hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam mbalimbali katika kuonesha ubantu wa
Kiswahili Massamba (1999) amewataja wataalam mbalimbali ambao wamehusika na
utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili, wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof
katika kitabu chake chaIntroduction to the phonology of the Bantu language,Duke
(1935 – 1945), Malcom Guthrie (1967), Dereck Nurse na Thomas Spear (1985). Hawa
walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu, kihistoria na
kiakiolojia.
Katikakigezo
cha kiisimu vipengele vinavyoangaliwa ni kama vile kufanana kwa msamiati wa
msingi, muundo wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia
mpangilio wa ngeli za majina.
Mizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za kibantu na Kiswahili
hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza kuonesha ukweli huu.
Mfano
Kiswahili
|
Kikurya
|
Kinyiha
|
Kijita
|
Maji
|
Amanche
|
Aminzi
|
Amanji
|
Jicho
|
Iriso
|
Iryinso
|
Eliso
|
Katika
mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana
kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano
wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.
Pia
mofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantu
hufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa maumbo ya maneno ya lugha ya
Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano, namna viambishi
vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika
katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya
mzizi na huwa na uamilifu bayana.
Mfano
Hebu
tuchunguze mifano ifuatayo:
Kiswahili
|
Kisukuma
|
Kisimbiti
|
Kinyiha
|
A-na-lim-a
|
a-le-lem-a
|
a-ra-rem-a
|
i-nku-lim-a
|
a-na-chek-a
|
A-le-sek-a
|
a-ra-sek-a
|
a-ku-sek-a
|
Kwa
kuangalia mifano hii utagundua kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata
kanuni moja kwamba mahali kinapokaa kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia
hukaa kwa upande wa lugha za kibantu, kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya
kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa kuna unasaba baina ya lugha hizi
Vilevile
sintaksia ya lugha ya Kiswahili na
lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi ya mpangilio wa vipashio na kuunda sentensi hufanana
yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana katika
Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi inakuwa na pande mbili
yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande wa kiima kipashio
chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio chake kikuu ni
kitenzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima nomino ianze na
baadaye kitenzi.
Mfano
Hebu
tuangalie mifano ifuatayo:
Kiswahili
|
Mama / anakula N (K) T (A)
|
Kijita
|
Mai / kalya N(K) T (A)
|
Kihehe
|
Mama/ ilya N(K) T(A)
|
Kihaya
|
Mama / nalya N(K) T(A)
|
Katika
mifano hii tumeona kwamba muunndo wa kiima-kiarifu katika lugha za kibantu
unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani nomino hukaa upande wa kiima
halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu, kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza
kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya lugha za kibantu.
Pia
mfumo wa sauti (fonolojia) wa lugha
za kibantu unafana sana na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika
kuunda silabi, na miundo ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha
ya Kiswahili hakuna muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na
konsonanti, muundo asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu
vilevile katika lugha za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi
zote huishia na irabu.
Mfano
Mifano
ifuatayo hufafanua zaidi:
Kiswahili
|
Baba
|
K+I+K+I
|
Kikurya
|
Tata
|
K+I+K+I
|
Kiha
|
Data
|
K+I+K+I
|
Kijita
|
Rata
|
K+I+K+I
|
Kipare
|
Vava
|
K+I+K+I
|
Tanbihi:
K= konsonanti I= irabu.
Kwa
mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana na
ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni
za familia moja.
Pia
vilevile mfumo wa ngeli za majina katika
lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji
wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha
ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa
neno, hivyohivyo katika lugha za kibantu
Kwa mfano:
Umoja
|
Wingi
|
|
Kiswahili
|
m-tu
|
wa-tu
|
Kikurya
|
mo-nto
|
abha-nto
|
Kiha
|
umu-ntu
|
abha-ntu
|
Kikwaya
|
mu-nu
|
abha-nu
|
Mifano
hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba vipashio vyote vya umoja na wingi
hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa
nasaba moja.
Vilevile
katikaupatanisho wa kisarufilugha za kibantu na Kiswahili huelekea kufanana
viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambishi vya nafsi.
Mfano wa viambishi vya nafsi
Kiswahili
|
Mtotoa-nalia
|
Kizanaki
|
Umwanaa-rarira
|
Kisukuma
|
Ng’wanaa-lelela
|
Kikurya
|
Omonaa-rakura
|
Tunaona
hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza katika
lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na
kibantu.
Pamoja
na ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili
pia kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na
kiethinolojia.
Ushahidi wa Kihistoria
Ushahidi
wa kihistoria huchunguza masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo
huelezea asili na chimbuko la wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile
ugunduzi wa kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa upwa wa
Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya
kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia, huchunguzwa tarihi
mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu wa pwani ya Afrika Mashariki na
lugha yao.
Kwa
ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na
wakazi wake wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia
maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa
ilikuwa ni Kiswahili.
Jinsi Miundo ya Kiswahili inavyofanana na Miundo ya Lugha nyingine za Kibantu
Miundo
ya lugha ya za kibantu inafanana na lugha ya Kiswahili na kufanana huko hutokea
katika miundo silabi ambapo zote huishia na irabu na siyo konsonanti, miundo ya
sentensi, miundo ya vitenzi vya Kiswahili ni sawa na ile ya Kibantu. Kwa mfano
vitenzi vya Kiswahili na kibantu vina uhusiano mkubwa hasa katika viambishi,
mnyumbaliko na pamoja na mianzo na miisho ya vitenzi. Mada hii imefafanuliwa
vizuri katika mada iliyotangulia hapo juu.
Katika
karne ya kumi na tisa Afrika Mashariki iliingia kwenye mahusiano na mataifa
mengine kama vile Marekani, Ujerumani na Uingereza. Mahusiano haya ni baada ya
watu wa pwani kuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na Waaarabu, hawa
waliweka athari kubwa katika kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Wageni
kutoka Ulaya walipoingia Afrika Mashariki walifanya biashara, shughuli za
kidini (mishenari), elimu na utawala. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha
Waarabu, uwepo wao pia ulikuwa na athari katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili
Afrika Mashariki na kwingineko.
Ukuaji wa Kiswahili
Kimsamiati nchini Tanzania katika Enzi ya Waarabu
Waarabu
hasa katika pwani ya Afrika Mashariki walifanya biashara ikiwemo biashara ya
watumwa. Ilikuwepo misafara mbalimbali ya biashara kutoka pwani hadi bara.
Katika misafara hiyo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasiliano hivyo
Kiswahili kikaenea pia katika sehemu za bara.
Kuna
mambo kadhaa waliyofanya waarabu ambayo yalichangia kukua kwa lugha ya
Kiswahili. Waarabu walichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:
Biashara
Waarabu
walifanya biashara kati ya pwani na sehemu za bara, katika biashara yao
walichangia kwa kiasi kikubwa uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kuu ya
mawasiliano na ya kibiashara iliyotumiwa na wafanya biashara wa kiarabu ilikuwa
ni Kiswahili, kwa hiyo kwa njia hii waliweza kueneza Kiswahili kuanzia pwani
hadi maeneo ya bara kama vile Tabora, Kigoma hadi mashariki mwa Kongo.
Dini
Dini
pia ni jambo ambalo liliweza kuchangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili enzi za
waarabu. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa
hivyo iliwabidi kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia, lugha
iliyokuwa ikitumiwa ni lugha ya Kiswahili. Na hivyo hii ikasaidia kuenea kwa
lugha ya Kiswahili.
Maandishi ya kiarabu
Waarabu
pia walileta hati zao zilizotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Kwa
hiyo kupitia hati za kiarabu maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili
yaliweza kuhifadhiwa, hivyo Kiswahili kiliweza kukua kwa vile kingeweza
kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.
Kuoana
Pia
vilevile Waarabu waliofika pwani waliweza kuoana na wabantu, hii ilisababisha
kizazi kipya kutokea. Na kwa sababu hiyo watoto walichukua maneno mengi kutoka
kwa baba na mama yao na hivyo kuongeza msamiati katika lugha Kiswahili.
Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Wajerumani
Wajerumani
waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875, walifanya kila
jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya biashara,
waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika shuguli zote
hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza
Kiswahili. Walipongia
katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha enea kwa kiasi
kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na kuenea kwa
Kiswahili kama ifuatavyo:
Kutoa mafunzo ya
lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali
Waliwalazimisha
wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa sababu sheria ilikuwa
ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika serekali ya mjerumani. Kwa
hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze
kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze Kiswahili ni pamona na
maakida. Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze
kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za
kiutawala.
Ujenzi wa shule
Shule
zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala
wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha
ya Kiswahili
Kuenea kwa utawala wa
Wajerumani nchi nzima
Utawala
wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya kazi wa serikali
ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo kila sehemu
palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.
Shughuli za kiuchumi
Pia
katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu
mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa
hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi
ilikuwa ni Kiswahili. Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani
ulitoa msukumo mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao
za kiutawala, hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.
Ueneaji wa Kiswahili
nchini Tanzania katika Enzi za Wajerumani
Wajerumani waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875,
walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya
biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika
shuguli zote hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na
kukiendeleza Kiswahili. Walipongia katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha
enea kwa kiasi kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na
kuenea kwa Kiswahili kama ifuatavyo:
Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa
wafanyakazi wa serikali
Waliwalazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa
sababu sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika
serekali ya mjerumani. Kwa hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha
ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze
Kiswahili ni pamona na maakida.
Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana
na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.
Ujenzi wa shule
Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika
utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa
ni lugha ya Kiswahili
Kuenea kwa utawala wa Wajerumani nchi nzima
Utawala wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya
kazi wa serikali ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo
kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.
Shughuli za kiuchumi
Pia katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu
mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa
hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi
ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani ulitoa msukumo
mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao za kiutawala,
hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.
Enzi za Wajerumani (Elimu) |
Elezea ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi za Wajerumani
Wajerumani walichangia kwa sehemu kubwa kuenea kwa lugha ya Kiswahili
nchini Tanzania enzi za utawala wao. Mambo yaliyochangia kuenea kwa lugha ya
Kiswahili enzi za utawala wa Wajerumani ni pamoja na dini, elimu, shughuli za
utawala na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.
love it its very helful to me as a student
返信削除I like this app coz helps me so much may Allah guarantee all of you a happy life and more mafanikio
返信削除Thanks
削除I like this !
返信削除this how we can make sure know what is wanted.
Ts is a very cool page and all thanks to the developer it helps a lot in studies and has got a full content of Tanzanian syllabus
返信削除Ilike it
返信削除