Close Menu
Msomi BoraMsomi Bora
    Msomi BoraMsomi Bora
    Button Login
    • NURSERY NOTES
    • PRIMARY NOTES
    • O-LEVEL NOTES
    • A-LEVEL NOTES
    • SOLVED EXAMS
    • PAST PAPERS
    • OTHERS
    Msomi BoraMsomi Bora
    • NURSERY NOTES
    • PRIMARY NOTES
    • O-LEVEL NOTES
    • A-LEVEL NOTES
    • SOLVED EXAMS
    • PAST PAPERS
    • OTHERS
    Kiswahili

    KISWAHILI: FORM TWO: Topic 3 – UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

    Msomi BoraBy Msomi BoraJune 5, 20184 Mins Read


    TOPIC 3: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

    Fasihi
    simulizi kama zilivyo kazi nyingine za fasihi andishi hufanyiwa uhakiki.
    Uhakiki huu huzingatia vipengele vya fani na maudhui ili kubainisha usanaa wa
    kazi husika pamoja na kile ilichokusudia kufikishwa kwa hadhira.
    UHAKIKI WA USHAIRI
    Mashairi
    kama kazi nyingine za kifasihi huhakikiwa kwa kutumia vigezo sawa na
    vinavyotumika katika kazi nyingine za kifasihi. Vigezo hivyo ni kwa kuzingatia
    vipengele vyake viwili yaani fani na maudhui.
    VIPENGELE VYA FANI
    Uhakiki
    wa fani za ushairi ni uchambuzi wa kina na kuziweka wazi mbinu za kisanaa
    alizotumia mshairi katika kutunga kazi yake. Vipengele muhimu vya kuhakiki
    katika fani ya ushairi ni kama vifuatavyo:
    Mtindo
    Jambo
    la kuonyesha hapa ni kwamba iwapo shairi ni la kimapokeo ama ni la kisasa.
    Muundo.
    Katika kuhakiki muundo wa shairi mhakiki inatakiwa aweke wazi mambo yafutayo:
    1.
    Idadi ya beti
    2.
    Idadi ya mistari na aina ya vibwagizo
    3.
    Idadi ya vipande
    4.
    Idadi ya mizani
    5.
    Aina na mpangilio wa vina

    Wahusika
    Ikiwa
    shairi limehusisha wahusika ni vema pia mhakiki awabainishe
    Matumizi ya Lugha
    Katika
    kipengele hiki mhakiki huchunguza:

    1.
    Mpangilio wa maneno. Mf. Wengi wari badala ya wari wengi

    2.
    Matumizi ya: Mazida – kurefusha neno
    mfano, kiwembe badala ya wembe; Ikisari – kufupisha neno mfano siombe badala ya usiombe; Tabdila – kubadilisha mwendelezo wa neno mfano
    kujitanuwa badala ya kujitanua.

    3.
    Matumizi ya methali, misemo na nahau

    4.
    Matumizi ya lugha ya picha

    5.
    Matumizi ya tamathali za semi kama vile takriri, sitiari n.k

    6.
    Mbinu nyingine za kisanaa

    Mhakiki
    anapochunguza vipengele vya fani, jambo muhimu la kuzingatia ni jinsi vipengele
    hivyo vinavyosaidia kuwasilisha maudhui.

    Ushairi


    VIPENGELE VYA MAUDHUI
    Ili
    kuhakiki na kupata maudhui ya shairi inatakiwa kulisoma shairi kwa kulielewa
    zaidi. Baada ya kupata picha fulani kuhusu shairi na kutafakari maana za maneno
    muhimu, itatubidi tuelewe vipengele vya maudhui, ambavyo ni dhamira, mtazamo,
    msimamo, falsafa ya mwandishi, ujumbe na maadili, migogoro na muktadha.
    UHAKIKI WA MAIGIZO
    Igizo
    huhakikiwa kwa namna lilivyo katika maumbo yake yote mawili yaani fani na
    maudhui.
    Vipengele vya Fani na
    Maudhui katika Kuhakiki Maigizo

    Fani
    Uhakiki
    wa fani katika maigizo unajihusisha na ufundi uliotumiwa. Ufundi huu
    unajumuisha mambo kadhaa kama ifuatavyo:
    Mtindo

    Mtindo
    ni sura ya maigizo inayojitokeza kupitia mpangilio wa maneno na vitendo.
    Inabidi mhakiki achunguze kama kazi ni:

    1.
    Mchezo wa jukwaani – wenye mpangilio wa mazungumzo baina ya watu na matendo
    yao.

    2.
    Majigambo


    3.
    Vichekesho – mpangilio wa maneno yanayowasilisha ujumbe kwa kuchekesha.

    4.
    Mazungumzo – maongezi ya kujibizana baina ya watu.

    5.
    Ngonjera – mpangilio wa tungo za kishairi ambapo watu wawili au makundi mawili
    hukinzana.

    6.
    Miviga – sherehe za kitamaduni kama vile matambiko

    Pamoja
    na haya, mtindo hutegemea lengo la maigizo ambalo laweza kuwa kuelimisha,
    kukejeli, kuburudisha, kuonya, kukosoa na kadhalika.
    Mandhari

    Mazingira
    ya kutendea ni kipengele muhimu cha fani. Mhakiki hana budi kujiuliza iwapo
    utendaji unadhihirisha wakati au mahali halisi. Jambo hili huweza kutekelezwa
    kupitia vifaa, maleba, maneno n.k.
    Wahusika
    Maswali
    ya mhakiki kuuliza ni:
    1.
    Wamejitokeza kikamilifu?
    2.
    Wanaaminika?

    Matumizi ya lugha
    Vigezo
    anavyotumia mhakiki kuchunguza lugha ni:

    1.
    Kama usemaji ni wa kisanaa, yaani unatumia picha, tamathali za semi, methali,
    nahau n.k.

    2.
    Kama lugha imetumika vile inavyotumiwa katika jamii. Mfano: kiimbo, mkazo,
    miguno, vihisishi n.k.

    3.
    Matumizi ya maneno ya ajabu kama yale yanayotumiwa na waganga.

    Maleba na vifaa

    Hivi
    huakisi mandhari na husaidia kuzua mukatadha. Kwa hiyo ni muhimu kuchunguza
    kama vimetumiwa ipasavyo.
    Matumizi ya ala

    Matumizi
    ya ala kama ngoma, baragumu, au sauti zingine ili kuamsha hisia za hadhira ni
    jambo muhimu kuchunguza.
    Mbinu nyingine

    Mhakiki
    anapaswa pia kuchunguza matumizi ya nyimbo, uchezaji ngoma, usimulizi na mbinu
    nyingine katika kuibua hisia za watazamaji.
    Maudhui

    Kwa
    upande wa maudhui, mhakiki wa maudhui hutakiwa kuchunguza vipengele vyote vya
    kimaudhui ambavyo ni dhamira, migogoro, maadili, mtazamo na msimamo wa fanani
    pamoja na ujumbe bila kusahau kipengele cha falsafa. Yote hayo kwa pamoja ndiyo
    humsaidia mhakiki kubaini ukinzani wa igizo na maisha halisi ya jamii ambayo huwa
    ndiyo hadhira ya igizo hilo.
     

    Maigizo

    Previous ArticleKISWAHILI: FORM TWO: Topic 2 – MATUMIZI YA LUGHA KATIKA MIKTADHA MBALI MBALI
    Next Article KISWAHILI: FORM TWO: Topic 4 – UHIFADHI WA KAZI YA FASIHI SIMULIZI
    Msomi Bora

    Related Posts

    Kiswahili Books for Secondary Schools – All Levels

    May 7, 2025

    A Guide to Pass Kiswahili – Necta Exams

    September 6, 2021

    Methali 1500 za Kiswahili na Maana zake

    May 5, 2021

    KISWAHILI: FORM THREE: Topic 4 – UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

    August 1, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR SECONDARY STUDENTS

    June 26, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR ADVANCED LEVEL – Form 5 and 6

    June 26, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR ORDINARY LEVEL

    June 26, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR FORM SIX – ALL TOPICS

    June 26, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR FORM FIVE – ALL TOPICS

    June 26, 2018

    KISWAHILI NOTES FOR FORM FOUR – ALL TOPICS

    June 26, 2018

    3 Comments

    1. Unknown on June 11, 2019 10:06 am

      i like science subject

      Reply
    2. Unknown on February 17, 2021 9:32 am

      Nimependa summary ya uhakiki wa ushairi na migizo

      Reply
    3. Unknown on March 16, 2022 5:33 pm

      Mbona hakuna uhakiki wa ngonjera

      Reply
    Leave A Reply Cancel Reply

    © 2025 Copyright. All Rights are Reserved. Msomi Bora.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.

    Sign In or Register

    Welcome Back!

    Login to your account below.

    Lost password?