Author: Msomi Bora

KISWAHILI NOTES FOR FORM FOUR(Kiswahili Kidato cha Nne) We have:Notes 1 and Notes 2Notes 1To view the Notes, click the following links below: TOPIC 1 – KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI TOPIC 2 – UENEAJI WA KISWAHILI ENZI ZA WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU TOPIC 3 – UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI TOPIC 4 – KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI TOPIC 5 – UANDISHI TOPIC 6 – UFAHAMUNotes 2To view the Notes, click the following links below:1. UUNDAJI WA MANENO2. KUKUA NA KUENEA KWA KISWAHILI ENZI YA WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU3. UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI4. UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI5. UANDISHI6.…

Read More

TOPIC 6: UFAHAMU UFAHAMU WA KUSIKILIZA Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe. Kujibu Maswali ya Habari Uliyosikiliza Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha: Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya…

Read More

TOPIC 5: UANDISHI UANDISHI WA INSHA ZA KIADA Insha ni kifungu cha maandishi kilichoandikwa kutokana na mtazamo wa mwandishi katika kujadili juu ya mada fulani. Mwandishi anaweza kuandika kuipinga mada hiyo au kuishadidia mada hiyo. Kuna aina mbili za insha, insha za kaida (zisizo za kisanaa) na insha za kisanaa. Insha za kaida ni insha zinazotumia lugha ya kawaida kuelezea mambo mbalimbali katika jamii, mfano juu ya mazingira, uchumi, biashara, historia n.k. Muundo wa Insha za Kaida Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo: 1. Kichwa cha insha; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako.…

Read More

TOPIC 4: KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI UTUNGAJI WA MASHAIRI Utungaji/uandishi wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka aliwasilishe wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma akilini mwake. Mambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja. 1. Kuona: je, mhusika…

Read More

TOPIC 3: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo: 1. Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi; Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana…

Read More

TOPIC 2: UENEAJI WA KISWAHILI ENZI ZA WAINGEREZA NA BAADA YA UHURU Ukuaji na Ueneaji wa Kiswahili katika enzi ya Waingereza Waingereza walipochukua koloni la Tanganyika kutoka kwa Wajerumani walikuta Kiswahili kimeimarika na kinatumika katika maeneo mengi ya nchi. Kwa kuwa nao walihitaji kutawala hawakupuuzia matumizi ya Kiswahili katika utawala wao japo hawakutumia Kiswahili kwa lengo la kukikuza lakini walijikuta wanakieneza na kukikuza bila ya wao kukusudia. Mambo waliyochangia Waingereza katika Ukuaji wa Kiswahili nchini Tanzania Waingereza walitumia Kiswahili kama nyenzo ya kusaidia shughuli zao za kiutawala. Hata hivyo kuna mambo waliyofanya waingereza yaliyosaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili, mambo…

Read More

TOPIC 1: KUONGEZA MSAMIATI WA KISWAHILI Uundaji wa Maneno Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe. Njia za Uundaji Maneno Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo: Kubadili mpangilio wa herufi. Kuambatanisha maneno. Kutohoa maneno ya lugha nyingine. Uambishaji wa maneno. Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura. Kuunda Msamiati kwa kubadili Mpangilio wa Herufi Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine Mfano…

Read More

KISWAHILI NOTES FOR FORM THREE (kiswahili Kidato cha Tatu)   We have: Notes 1 and Notes 2   Notes 1 To view the Notes, click the following links below: TOPIC 1 – NGELI ZA MANENO TOPIC 2 – MJENGO WA TUNGO TOPIC 3 – MAENDELEO YA KISWAHILI TOPIC 4 – (a) UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI (Utangulizi, Maelezo)                  (b) UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI (Riwaya, Tamthiliya, Ushairi) TOPIC 5 – UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI TOPIC 6 – UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO TOPIC 7 -…

Read More

TOPIC 7: KUSOMA KWA UFAHAMU KUSOMA KIMYA Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti. Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyosoma Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo: 1. Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatkiwa ajiluze, Je, kinachoongelewa hapa nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo. 2. Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo…

Read More

TOPIC 6: UANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO UANDISHI WA INSHA ZA KISANAA Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira. Au, Insha ya kisanaa ni ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali za semi.…

Read More